Maria Mpangala Mama Mzazi wa mrembo Geneviv, akimbusu kwa furaha mwanae bada ua kutangazwa na kuvishwa taji la Vodacom MISS Tanzania 2010.
Vodacom Miss Tanzania 2010 Geneviv Mpangala (katikati) akiwa na washindi wenzake msindi wa pili, Glory na Consolata, baada ya kutangazwa washindi katika kinyang’anyiro hicho kilichofanyika katika uku bi wa Mlimani City Mwenge Jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo
Vodacoma Miss Tanzania 2010, Geneviv Mpangala, akipita na kupunga mkono kwa furaha baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaaam.
Majaji wa shindano hilo wakiwa makini kufuatilia shindano hilo…
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, wakifurahia jibu la Mrembo Pendo, aliyemfagilia Rais Jakaya Kikwete wakati akijibu swali lake aliloulizwa.
Warembo waliofanikiwa kuingia nafasi tano bora ikiwa ni fainali ya kumpata Vodacom Miss Tanzania 2010, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi…
Warembo waliofanikiwa kuingia nafasi kumi bora wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa…
"Oyaa nyanyuka twende wewe jikaze mtoto wa kike unachekwa"
Mrembo akianguka jukwaani wakati akipita na wenzake na vazi la ufukweni Duh aibu we acha tuuu.
Warembo wakipita jukwaani na vazi la Ufukweni….
Msanii Lina na mwenzake wote kutoka THT, wakishambulia jukwaa…
Wasanii wa Tanzania House of Talent THT, wakishambulia jukwaa, wakati wa shindano hilo…
Warembo wakipita jukwaani na vazi la Ubunifu……
Mapaparazi nao hawakuwa nyuma katika kuhakikisha wananasa picha za kila tukio, lakini eti hakuna hata mmoja kati ya hawa aliyepata picha ya mrembo aliyeteleza na kuanguka jukwaani……







No comments:
Post a Comment