Mkurugenzi wa Kampuni ya Indoma, Masoud Salim |
Indoma Tours, ni kampuni inayomilikiwa na vijana ambayo inajali zaidi maslahi yao na kuwawezesha kuwa na misingi bora ya kimaisha, ambapo imekuwa ikiwasaidia vijana wengi sana kuachana na madawa ya kulevya na mambo mengine yasiyofaa katika jamii.
Kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana na vijana wa 'Sober House' mara kwa mara na kutoa misaada ya hali na mali kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuendeleza mshikamano baina yao , Vijana na Jamii kwa ujumla.
Katika kuendeleza urafiki huu, Wafanyakazi wa Indoma 'Staff' na vijana wa Rehab au ‘Mateja’ kama wanavyopendelea kujiita, watakutana katika mchezo wa kirafiki siku ya jumapili ya Feb 24, saa kumi jioni, katika viwanja vya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar, ili kubadilishana mawazo na kujenga ushirikiano na umoja ikiwa ni sehemu ya kuwafundisha vijana watumiaji wa madawa ya kulevya stadi za kazi.
Kabla ya mchezo huo Kampuni ya Indoma itaongozana na timu zote mbili na kutembelea, Sober House, na kukabidhi msaada wa vyakula wenye thamani ya Sh. 500,000/= kwa waathirika hao.
Drug Free Zanzibar, wameanzisha nyumba za sober houses hapa visiwani, ambapo watumiaji wa madawa ya kulevya wamekuwa wakipatiwa mafunzo ya miezi minne ili kuachana na madawa ya kulevya.
Kwa kutambua umuhimu wa Drug Free Zanzibar, Kampuni ya Indoma imeamua kufanya kazi kwa ukaribu na Drug Free Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya kuwasapot kwa kazi yao nzuri.
'Sisi Indoma tunatambua mazingira ya Visiwani Zanzibar na pia tunawatambua vijana wa Visiwani hapa, ndiyo maana tumeamua kufanya kazi katika mazingira ya Zanzibar ili kuwasidia vijana waliopotea kwa kujiingiza katika janga la utumiaji wa madawa ya kulevya, na vijana ni sehemu ya Jamii inayotuzunguka kwa hiyo kama vijana wetu hatuwezi kuwatenga, tunasimama bega kwa bega nao kuwaonesha njia ili waweze kujikomboa kuachana na madawa ya kulevya''.alisema Mkurugenzi wa Kampuni ya Indoma, Masoud Salim
No comments:
Post a Comment