Mfuko
wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) umekamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi
wa nyumba 641 katika mikoa mitano ambazo zilianza kuuzwa tangu Novemba mwaka
2012. Mradi huo unalenga kutatua tatizo la makazi kwa wanachama wake na jamii
kwa ujumla.
Mikoa
iliyojengwa nyumba hizo na idadi ya nyumba katika mabano ni Dar es salaam –
Buyuni (491), Morogoro – Lukobe (25), Shinyanga – Ibadakuli (50), Tabora –
Usule (25) na Mkoa wa Mtwara – Mang’amba (50).
Aidha
kwa Mujibu wa maelezo ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bwana Adam Mayingu, amewaambia wanaadishi wa habari na viongozi mbalimbali waliotembelea eneo la
mradi huo Mkoa wa Dar es Salaam kuwa Shirika lake limejenga nyumba za aina nne
ambazo ni za nyumba viwili, Vyumba vitatu, Nyumba za vyumba vitatu kimoja kikiwa
ni Master na Nyumba ya vymba vine kimoja kikiwa ni Master.
Gharama
ya ununuzu wa nyumba hizo ambazo zinauzwa kwa wanachama wa Mfuko huo ni kati ya
Shilingi Milioni 64 hadi milioni 94 gharama zikijumlishwa na Kodi ya ongezejo
la Thamani.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu
(katikati) akiwaonesha maofisa wa Jeshi la Polisi moja ya nyumba 491 zilizopo
katika mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ambazo zitkopeshwa kwa
wanachgama wa mfuko huo. Nyumba hizo zipo katika eneo la Kigezi Kata ya Majohe
wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu
(kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa
ziara hiyo ya kuakagua makazi hayo. Kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya
Ilala, Hery Mohamed Kessy Nyumba hizo zipo katika eneo la Kigezi Kata ya Majohe
wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wakitembelea nyumba hizo hii leo.
Ziara ikiendelea katika nyumba hizo zipatazo 491
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu
akiwa eneo la jikoni katika moja ya nyumba hizo.
Vigezo
vya kununua nyumba hizi ni lazima uwe mwanachama ambaye umechangia makato kwa miaka
mitano na zaidi na awe amesajiliwa na mfuko, Lakini pia nyumba hizi zinauzwa
kwa fedha taslimu au kwa kutumia nusu ya mafao ya mwanachama kwa wale walio
bakisha miaka 5 kustaafu.
Faida
kubwa ambayo Mkurugenzi wa PSPF amesema mnunuzi wa nyumba hizi ataipata ni kuwa
Nyumba atakayo nunua imekamilika na imejengwa katika uwanja wa ukubwa wa Sqm 800-2500,
nyumba ipo katika eneo rasmi lililopimwa na unaweza kupata mkopo wa Benki kwa
riba ya asilimia 12.
No comments:
Post a Comment