Habari za Punde

*KOCHA WA MAN U SIR ALEX FERGUSON ATANGAZA RASMI KUJIUZULU


KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, ametangaza kujiuzulu rasmi huku akiwa ametwaa mataji zaidi ya 30 katika miaka yake 26 ya kuinoa Manchester United, vikiwamo vikombe 13 vya Ligi Kuu ya England, anatarajia kuaga mashabiki katika mechi ya mwisho ya ligi ya msimu huu, ugenini dhidi ya West Bromwich Albion, Mei 19.
Ferguson anatarajia kustaafu, kuhitimisha zaidi ya robo karne ya kufanya kazi Old Trafford, klabu hiyo imetangaza rasmi leo Jumatano, Jijini London.
Fergie, (71) ameiongoza Klabu kwa mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja, akiingiza klabu hiyo katika soko la hisa la New York Stock Exchange, huku ikikusanya mamilioni ya mashabiki duniani kote kuanzia mwaka 1986 aliposhika usukani wa kuiongoza klabu hiyo.
Katika miaka yake 26 ya kuinoa Man United, Ferguson raia wa Scotland, ametwaa zaidi ya mataji 30, yakiwamo 13 ya Ligi Kuu ya England – ikiwa ni pamoja na ubingwa wa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.