Habari za Punde

*MAJAMBAZI YAUA MWANAMKE KWA RISASI DAR NA KUMPORA SH. M 10


Majambazi yasiyojulikana leo majira ya saa 11 jioni, yamempiga risasi na kumuua mama mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja na kisha kumpora kiasi cha fedha Sh. milioni 10 .
Mashuhuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu kuwa Marehemu huyo, aliyeuawa alikuwa akitoka benki ya CRDB tawi la Uhuru, ambapo majambazi hao waliokuwa wakimfuatilia wakiwa na pikipiki waliligonga gari lake kwa makusudi na ndipo dada huyo aliposimama ili kujua tatizo la kugongwa na watu hao.
Wakiendelea kusimulia walisema kuwa baada  tu ya dada huyo kutelemka garini kwake, Majambazi hao mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kuingia garini kwa dada huyo na kisha kutoka na mkoba wake unaosemekana ulikuwa na kiasi cha fedha Sh. milini 10, na kutokomea nazo kusikojulikana huku wakiwaacha watu wakikusanyika eneo la tukio kujua kilichotokea na wengine wakijaribu kumsaidia marehemu huyo ambaye alifariki dunia papo hapo.
KWA SABABU ZA KIBINADAMU MTANDAO HUU UMESHINDWA KUTUMIA PICHA ILIYOUFIKIA MTANDAO KUTOKANA NA TASWIRA YENYEWE......TUNAWAOMBA RADHI WASOMAJI WETU 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.