Habari za Punde

*MASHINDANO YA MBIO ZA MBUZI ZA HISANI 2013 ZA DAR ZAKARIBIA


 Mbuzi wakichuana ili kumpata mshindi katika mwashindano ya mbio za mbuzi za hisani za mwaka jana. (Picha ya Maktaba)
*****************************************************
‘Mbuzi Mmoja tu, Anaweza Kuleta Mabadiliko’  
Waandaji wa mbio hizo maarufu nchini wamesema jijini hapa leo kuwa kwa sasa mbuzi watakaoshiriki mbio hizo wako kwenye kambi za mazoezi huku zawadi kemkem za kuvutia zikiwa zimeandaliwa kwa mwaka huu.

“Tunachokihitaji kwa sasa ni uwepo wa mashabiki watakaohudhuria tukio hilo la kufurahisha na hivyo kutusaidia kufikia lengo tulilojiwekea la kusanya shilingi bilioni moja kwa ajili ya taasisi mbalimbali za kujitolea nchini,” Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Mama  Karen Stanley alisema.


“Siku hiyo tumeandaa sehemu mahsusi kwa ajili ya aina mbalimbali ya vyakula vya kuvutia kutoka sehemu maarufu zinazohusika na mapishi jijini Dar kama Rose Garden, Arca di Noe, Black Tomato na Q Bar.

“Pia tutakuwa na eneo lililokarabatiwa kwa ajili ya michezo ya watoto litakalowafanya watoto watakaofika kufurahi na kuikumbuka siku hiyo. Lipo eneo jingine jipya kwa watoto wadogo zaidi huku eneo jingine lililotayarishwa na Neverland Playgroup and entertainment kwa ajili ya watoto wakubwa zaidi litakalokuwa na michezo kama sarakasi, ngoma, kucheza muziki na wachekeshaji kutoka asasi ya  Kigamboni Community Centre.”


Tukio hilo ka kifamilia la kila mwaka litafanyika Juni Mosi mwaka huu kwenye eneo la Green, mtaa wa Kenyatta kuanzia saa sita mchana hadi saa 11.30 jioni. Gharama za tiketi ni Sh 5,000 kwa watu wote na zitauzwa getini.

Mbio hizo za mbuzi za hisani zinafanyika kwa mara ya 13 mwaka huu. Tangu yalipoanzishwa mwaka 2001, tayari zaidi ya shilingi milioni 660 zimekwisha kusanywa kwa ajili ya mashirika na taasisi mbalimbali za kujitolea nchini.  

Mwaka jana tukio hilo liliweka rekodi kwa kukusanya shilingi milioni 115 kwa kwa ajili ya mashirika 15, huku wahudhuriaji wakifika 4,200 na kulipa kiingilio getini.

Mama Stanley alisema: “Mwaka huu tunatarajia kufanya makubwa zaidi. Tunafuraha ya kuwa na wadhamini wengi muhimu sana, ambao ndio uti wa mgongo wa tukio lenyewe. Bila wao hakika tusingekuwa hapa. Kwa namna ya pekee yunatoa shukrani kwa wadhamini wa mbio hizo Southern Sun, Coca-Cola, Tanzanian Breweries Limited, Mantra Tanzania, Erolink, FNB na Symbion.

“Lakini ukweli ni kwamba bila ujio wa watu wa kawaida, mashabiki kutoka sehemu mbalimbali za Dar, wenyeji na wageni, kushuhudia mbio hizo za aina yake kusingekuwa na maana yoyote. Kwa hiyo karibuni nyote, msiisahau siku hiyo ya ajabu kabisa!”

Miongoni mwa zawadi kubwa kwa mwaka huu ni tiketi ya kwenda Ulaya na kurudi itakayotolewa na SWISS, safari ya kwenda kwenye mbuga ya wanyama ya Selous na kifurushi cha kupata mtandao wa Intaneti  kwa mwaka mzima kutoka UhuruOne kikiambatana na vifaa na uunganishaji.

Dhana ya mwaka huu, ‘Viumbe wa Baharini na Mabaharia’, inaweza kuvutia wengi wanaopenda kuingia kwenye mashindano ya mavazi ya kuvutia huku kukiwa na zawadi nono kwa kundi litakalovaa vyema. Kutakuwa pia na shindano la mavazi maalumu kwa watoto na zawadi kwao.

Mama Stanley alisema: “Ukija umevaa kwa mtindo wa nguva au baharia, au hata ukiwa kawaida tu utafurahia mambo tuliyokuandalia mwaka huu.”

Kwa habari zaidi tembelea tofutti yetu; www.goatraces.com

 Kwa waandishi wa habari wasiliana na Peter Mgongo kwa simu namba 0784 765454 au mgongo@gmail.com

Kwa maelezo yote kuhusu masuala ya habari wasiliana na Emma Pearson (Mjumbe wa Kamati anayeshughulikia masuala ya Habari na Mahusiano)  simu 0768 912933 au ekpea@yahoo.co.uk

Maelezo kwa Wahariri:

  1. Mwenyekiti wa Kamati ya ‘Goat Races’, Karen Stanley anapatikana kwa mahojiano ikiwa atahitajika.
  2. Picha pia zinapatikana kwa maombi rasmi.
  3. Jinsi mbio hizo zinavyofanyika:
Kuna aina saba za mashindano. Kila moja hudhaminiwa na wamiliki wa mbio hizo ambao kwa mwaka huu ni:
The Marvelous Mantra Mile
The Southern Sun Fillies Frolic
The Symbion Sweepstakes
The Kilitime Stakes
The Erolink Racy Recruits
The FNB Champions Cup
The Coca-Cola Open Happiness Sweepstakes
Hawa humlipia mbuzi mmoja katika shindano moja. Mbuzi wao akishinda, wanakuwa na nafasi ya kupata zawadi kubwa. Wengi huungana na rafiki au jamaa zao na kuwa wamiliki wa pamoja wa mbuzi.

Wote hupata nafasi ya kuingia kwenye eneo maalumu na kupata nafasi nzuri ya kumshangilia mbuzi wao, na kupata vinywaji na chakula bure kwa hisani ya Southern Sun Hotel, Tanzania Breweries Ltd, Tanzania Distilleries Ltd, na Coca-cola.

4      Mbio hizi zilianza jijini Dar es Salaam mwaka 2001 shukrani kwa muasisi Paul Joynson-Hicks. Alipata wazo hilo kutoka Uganda ambako wafanyabiashara walibuni wazo hili ili kukusanya fedha za hisani.

Zawadi maalumu kwa mwaka huu za bahati nasibu:

  1. The Raffle Prizes 2013 – tiketi ni Sh 2,500 na zitauzwa siku hiyo.
·         SWISS – tiketi moja ya kwenda na kurudi Ulaya
·         Selous Great Water Lodge – safari ya Selous
·         UhuruOne – kuunganishwa na internet ya bure kwa mwaka mzima
·         Sea Cliff Resort and Spa, Zanzibar – malazi hoptelini hapo kwa watu wawili na tiketi mbili za kwenda na kurudi Zanzibar kutoka Coastal Airlines
·         Benetton Gems – heleni za Tanzanite zenye thamani ya dola 1,000

·         Ras Kutani – malazi ya siku mbili
·         Arena Gym (zawadi mbili)  – uanachama wa gym kwa mwezi mmoja, massage ya saa moja pale Arena Spa na huduma za Saluni.
·         Anantara Spa – massage kwa mtu na mwenza wake
·         Toyota Tanzania – goodie bag
·         The Fitness Centre – uanachama wa gym kwa miezi mitatu
·         Akemi Revolving Restaurant – vocha ya chakula cha jioni ya thamani ya sh 250,000
·         Shrijees Supermarket – zawadi mbalimbali
·         TDL – zawadi mbalimbali

1.   Vituo vitakavyofaidika na mbio za mwaka huu ni:

  • Bibi Jann's Centre –
  • Fahari Zanzibar –
  • AC-AF –
  • Foxes' Community and Wildlife Conservation Trust –

  • The Daughters of Mary Immaculate and Collaborators (DMI)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.