Habari za Punde

*BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA MADAWATI 100 KWA SHULE ZA MSINGI 2 ZA ZANZIBAR

Meneja Masoko wa Benki ya NMB, Shilla Senkoro (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 10/- mke wa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha Balozi, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi madawati hayo yaliyotolewa na benki ya NMB. Makabidhiano hayo yalifanyika mwanzoni mwa wiki iliyopita Mjini Unguja. 
 Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya msingi Bumbwini na Mangapwani, wakiwa wamekaa kwenye madawati kwa furaha baada ya kukabidhiwa madawati hayo na Benki ya NMB kama msaada ili kupunguza uhaba wa madawati unaozikabili shule nyingi nchini Tanzania.
*******************************
Benki ya NMB imeendelea  kuwa karibu zaidi na jamii inayoizunguka kwa kusaidia kutatua matatizo mbalimbali  yanayoikabili jamii hususani  katika sekta ya elimu. 
Kama ilivyo ada kwa benki ya NMB  hutoa sehemu ya faida yake ili kuisaidia jamii.  
Benki ya NMB imetoa msaada wa madawati yenye thamani ya shilingi milioni 10/- kwa ajili ya shule ya msingi Mangapwani na Bumbwini mjini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.