Magari yakiwa katika foleni eneo la Kijitonyama mbele ya Millenium Tower, kutokana na eneo hilo kujaa maji ya mvua kubwa zilizonyesha jijini Dar es Salaam, juzi.
**************************************
Na Immaculate Makilika- Maelezo
SERIKALI imesema inatekeleza miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam yenye thamani ya sh. bilioni 876.336 katika barabara ya Al Hassan Mwinyi ambapo watumiaji wa barabara hiyo hutumia takribani saa moja na nusu kufika Osterbay polisi hadi daraja la Salender hususani mida ya asubuhi saa moja hadi saa tatu.
Hayo yalisemwa jana Bungeni na Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge Naibu wakati akijibu swali Mbunge wa Jimbo la Temeke Abasi Zuberi Mtemvu lililouliza kuwa Je,Serikali inaweza kutoa ufafanuzi juu ya ufumbuzi wa tatizo la msongamano huo?
Alisema kuwa inayolenga kutatua tatizo hilo ,ikiwemo miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo ambayo ni kama ifuatavyo;.Barabara ya Kimara –Kivukoni (fire),Fire-Kariakoo na Magomeni –Morocco (Sh. bilioni 240),Karakana na vituo vya mabasi yaendayo kwa haraka (BRT) pamoja na kuhamisha nguzo za umeme(sh. bilioni 47.90).
Nyingine ni Barabara ya Mwenge – Tegeta(sh. bilioni 88.00),Barabara ya Kilwa (Kilwa Road) Bendera Tatu-Mbagala Rangi Tatu ,(sh. bilioni 35.16),Daraja la Kigamboni (sh. 214.64).Flyover ya TAZARA,Serikali ya Japani imetoa msaada wa fedha kwa ajili ya usanifu,.Barabara ya Gerezani (Bendera –Tatu-KAMATA),Serikali ya Japani imetoa msaada wa fedha kwa ajili ya ujenzi.
Barabara ya Mandela (sh. bilioni 61.25) na.Barabara ya Wazo Hill –Bagamoyo-Msata (sh. bilioni 89.61).
Waziri huyo alisema ujenzi wa mabasi yaendayo haraka(BRT) kutoka Morocco kwenda Magomeni hadi Kivukoni na Kimara yatapunguza msongamano wa magari kati ya Osterbay Polisi na Daraja la Salender.
Aliongeza kuwa katika mipango ya baadae ,Serikali itaangalia uwezekano na kujenga barabara ya juu (viaduct) pande zote za daraja ,kujenga daraja lingine pembeni mwa daraja la Salender au kujenga njia mbadala (salender bridge Bypass) kutokea Kenyata Drive kuunganisha na Ocean Road.
* SERIKALI KUFUFUA KILIMO CHA KAHAWA KILIMANJARO
* SERIKALI KUFUFUA KILIMO CHA KAHAWA KILIMANJARO
SERIKALI imesema kuwa imeandaa mkakati wa kuendeleza tasnia ya kahawa ( Tanzania Coffee Industry Development Strategy,2012-2022) kwa lengo la kuendeleza kilimo cha zao hilo nchini kupitia Bodi ya kahawa nchini na kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya hiyo.
Aidha Serikali imefafanua kuwa hatua hiyo ni kuongeza uzalishaji ,tija na ubora wa kahawa Kitaifa ili kuboresha mapato ya wakulima wa zao hilo katika mikoa mbalimbali inayolilima ikiwemo mkoa wa Kilimanjaro .
Kauli hiyo ilitolewa leo Bungeni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Mahusiano na Uratibu Steven Wassira kwa niaba Waziri wa Kilimo ,Chakula na Ushirika , Chrisopher Chiza , wakati akijibu swali la Grace Kiwelu(Mbunge Viti Maalum-CHADEMA) aliyeuliza Je,Serikali ina mpango gani madhubuti na mahsusi wa kufufua kilimo cha Kahawa mkoani Kilimanjaro ambacho kwa miaka mingi kimekua tegemeo kwa wananchi wa Kilimanjaro na mhimili mkubwa kwa uchumi wetu wa Taifa letu.
Alisema malengo mahsusi ya mkakati huo ni pamoj ana kuongeza na uzalishaji wa kahawa safi kutoka wastani wa sasa wa tani 50,000 kwa mwaka hadi kufikia tani 100,000 ifikapo mwaka 2022 na kuongeza ubora wake ili kupata bei ya ziada katika masoko ya nje kutoka wastani wa asilimia 35 hadi kufikia wastani wa asilimia 70 ifikapo mwaka 2022.
Aidha Wassira alisema maeneo muhimu katika mkakati huo ni pamoja na kuimarisha huduma za ugavi ili wakulima wazingatie kanuni bora za kilimo,kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kahawa (TaCRI) ili kuhakikisha upatikanaji wa miche bora ya kahawa ,pamoja na kuongeza matumizi ya viwanda vya kati vya kuitayarisha ili kuongeza ubora wa zao hilo na hivyo wakulima kunufaika na bei nzuri.

No comments:
Post a Comment