Habari za Punde

*ZIARA YA MAKAMU WA CCM DK.SHEIN,WILAYA MICHEWENI PEMBA

 Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,na Viongozi wengine alipowasili katika uwanja wa Ukumbi wa Jamhuri Hall Wete Pemba leo katika mkutano wa kuwakabidhi kadi wanachama wapya 50 waliojiunga na Chama hicho katika ziara ya kuimarisha chama Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Wanachama na Wananchi wa Tawi la CCM Kipangani Wete,baada ya kuweka jiwe la msingi Tawi hilo,katika ziara ya kuimarisha Chama katika Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Iddi Thabit IT akitoa burudani yake kwa wimbo maalum aliotunga wakati wa Ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa na mazungumzo na wananchi na wanachama katika Tawi la CCM Kipangani Wete, katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba,katika uwanja wa Jamhuri Hall Wete leo.

 Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi Kadi mwanachama Mpya wa CCM Fatma Suleiman Said,akiwa katika miongoni mwa Wanachama 50 aliowakabidhi kadi leo,akiwa katika ziara  ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba.
 Mwanachama Mpya aliyejiunga na CCM Amour Suleiman,akijitambulisha kwa wanachama wa CCM Wilaya ya Wete,akifanya idadi ya wanachama Sitini na Moja waliojiengua Chama cha CUF,wakati wa Mkutano allioufanya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa katika ziara ya kuimarisha Chama katika Wilaya hiyo leo,baada ya kuweka jiwe la msingi tawi la CCM Kipangani.
Wasoma Utenzi wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa kaskazini Pemba Fatma Juma Ramadhan,(kushoto) na Halima Juma Haji,wakihani utenzi wao  kutoa burudani wakati wa mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipozungumza na wananchi na wanachama katika ziara ya  kuimarisha Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba,katika uwanja wa Jamhuri Hall Wete leo.Picha na Ramadhan Othman Ikulu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.