Habari za Punde

*TAIFA STARS KUREJEA KESHO JIONI KUTOKA NAMIBIA

KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinatarajia kurejea nchini kesho (Machi 7 mwaka huu) kutoka Windhoek, Namibia kwenye mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA.

Taifa Stars ambayo katika mechi hiyo dhidi ya Namibia (Brave Warriors) ilitoka sare ya bao 1-1 itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) majira ya saa 12: 45 jioni. badala ya muda wa awali wa 8: 15 mchana kwa ndege ya South Africa Airways.

Timu inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager baada ya kuwasili itakwenda hoteli ya Accomondia kwa ajili ya chakula cha mchana na baadaye kuvunja rasmi kambi yake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.