Adam Kuambiana enzi za uhai wake.
Msanii mahiri wa filam nchini, Adam Kuambiana, amefariki dunia alfajili ya kuamkia leo wakati akipelekwa kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam.
Aidha imeelezwa kuwa marehemu kuambiana, kabla ya kufikwa na umauti alikuwa akilalamika kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa tumbo baada ya kuanguka ghafla chooni wakati akiwa katika harakati za kurekodi 'Location' katika hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remmy, jijini Dar.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie, wakibeba mwili wa marehemu, Kuambiana kuutoa katika Hospitali ya Mama Ngoma, kupeleka Hospitali ya Muhimbili.
Wasanii wakilia kwa uchungu wa kuondokewa na mwenzao walipofika Hospitali ya Mama Ngoma.
Hospitali alipofia Kuambiana....
Ni kilio tu kwa wasanii.....




kila nafsi itaonja mauti innalillah wainna ilayhi rajiun!
ReplyDeleteduh kweli binadamu we are nothing in this world, jamani MUNGU alilaze roho ya marehemu mahala pema peponi. amina
ReplyDelete