Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipa kodi toka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard
Kayombo akionesha kwa waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam moja ya CD
zilizokamatwa wakati wa msako wa kubaini wale wote wanaojihusisha na uuzaji na
usambazaji wa kazi za wasanii bila kuwa na stempu za kodi katika bidhaa za
filamu na muziki. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo na
mwisho kulia ni Afisa Habari wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bi Mariam Mwayera.
Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipa kodi toka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard
Kayombo (katikati) akitoa wito leo Jijini Dar es salaam kwa wasambazaji na wauzaji wa kazi za Filamu
na muziki kuzingatia sheria na Kanuni zinazosimamia sekta hiyo kwa kuwa Serikali
itawachukulia hatua kali wale wote watakaoenda kinyume cha sheria na taratibu
zilizopo ikiwemo kutozwa faini isiyopungua milioni tano au kifungo
kisichopungua miaka mitatu jela. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi
Joyce Fissoo,Kushoto ni Afisa Utamaduni wa Bodi ya filamu Bw. Wilhadi Tairo.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo
akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mikakati ya
Bodi hiyo kuhakiksha kuwa kazi za wasanii wa filamu zinaendana na maadili ya
Taifa.kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania Bw. Richard Kayombo.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Filamu Tanzania ukilenga kueleza Mikakati ya Serikali katika kulinda haki za wasanii wa filamu na Muziki zinalindwa.
Picha na Frank Mvungi- Maelezo
*********************************************
Na Fatma Salum, MAELEZO
Serikali
kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeahidi kuendeleza msako wa
wafanyabiashara wote wanaouza kazi za filamu na muziki bila kubandikwa stempu
halali za kodi ili kuzilinda kazi hizo kwa ajili ya kuwanufaisha wasanii na
kuhakikisha Serikali inapata mapato yake.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma kwa Mlipa Kodi kutoka TRA Richard Kayombo
wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Kayombo
amesema TRA kwa kushirikiana na wadau wa tasnia ya muziki na filamu imedhamiria
kuhakikisha kuwa bidhaa za filamu na muziki zenye stempu za kodi ndizo
zinazoingizwa sokoni ili kulinda kazi za wasanii wa taifa letu dhidi ya dhuluma
zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiashara.
“Msako
huu endelevu utahusisha kukamata bidhaa zote ambazo hazijabandikwa stempu za
kodi na kuwachukulia hatua wahusika kwa mujibu wa sheria.” Alieleza Kayombo.
Aidha
Kayombo amefafanua kuwa kwa kipindi cha mwezi Februari na Machi 2016, TRA kwa
kushirikiana na Dalali wa Mahakama Yono Auction Mart & Company Limited
ilifanya msako jijini Dar es Salaam na kukamata jumla ya CD na DVD zenye
thamani zaidi ya shilingi Bilioni 1.3 ambazo zilisambazwa bila kufuata sheria
hivyo kukwepa kodi ya ushuru ipatayo shilingi Milioni 31.9 na gharama za stempu
zaidi ya shilingi Milioni 11.1.
TRA
inawatahadharisha wale wote wanaosambaza na kuuza kazi za filamu na muziki
ambazo hazijabandikwa stempu kuacha mara moja na kufuata utaratibu wa kupata
stempu hizo katika ofisi za TRA ili wawe na uhalali wa kuuza bidhaa hizo
kinyume chake hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
No comments:
Post a Comment