Habari za Punde

SERIKALI YAIFAGILIA BENKI YA NMB KWA KUTOA KWA JAMII

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndatwa Ngwilabuzu (katikati) akipokea sehemu ya Madawati, Viti na Meza vyenye thamani ya Tsh. milioni 20, kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar, Donatus Richard, wakati wa hafla ya makabidhiano hayo kwaajili ya Shule tatu za Sekondari za Buguruni Moto, Misitu na Umoja. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Shule Sekondari Buguruni Moto jijini Dar es Salaam, jana. Kushoto ni Meya wa jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto (wa pili kushoto) ni Diwani wa Kata ya Buguruni, Bosoro Pazi (wa nne kulia) ni Mkuruguenzi wa jiji la Dar es Salaam, Jumanne Shauri. 
**************************
SERIKALI imeitaja Benki ya NMB kama taasisi kiongozi nchini katika matumizi sahihi ya Programu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), inakotumia fungu lake kusapoti harakati za kukuza elimu na kuongeza ufaulu mashuleni, sambamba na kutatua changamoto zinazoikumba Sekta ya Afya.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng’wilabuzu Ludigija, wakati akipokea misaada yenye thamani ya Sh. Mil. 20, iliyotolewa na NMB, kwa ajili ya Shule za Sekondari Buguruni Motto, Shule ya Sekondari Misitu na Shule ya Msingi Umoja zilizoko wilayani Ilala.
Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika Ijumaa Juni 24, katika viwanja vya Shule ya Sekondari Buguruni Motto, ambako Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, alimkabidhi DC Ludigija mbele ya Meya wa Jiji, Omari Kumbilamoto na Mkurugenzi wa Jiji, Jumanne Shauri.
Akizunguma katika hafla hiyo, DC Ludigija alisema kuwa, NMB imekuwa taasisi kinara wa uungaji mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto na kuboresha miundombinu ya elimu na afya nchini, na kwamba shule, zahanati, vituo vya afya na hospitali zilizoko Ilala ni wanufaika namba moja wa CSR ya benki hiyo.
“Misaada hii ikawe chachu ya ufaulu kwa shule hizi na nichukue nafasi hii kusema kuwa NMB ni kinara wa matumizi sahihi ya sehemu ya pato lao wanalorejesha kwa jamii. Haijawahi kuchoka kusaidia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kwa hakika benki hii ni mfano wa kuigwa katika Sekta ya Kibenki,” alisema.
Alibainisha kuwa wanaipongeza benki hiyo namna inavyoshirikiana na Serikali katika kuzitupia macho na kuzitafutia ufumbuzi changamoto za elimu na afya, ambazo ni nyingi na haziwezi kumalizwa na Serikali pekee, bila nguvu ya wadau kama benki hiyo, huku akiyataka mashirika, makampuni na taasisi kuiga kwa NMB.
Kwa upande wake, Donatus, ambaye alikabidhi msaada wa meza na viti 150 na madawati 50 kwa DC Ludigija, alisema NMB imetenga kiasi cha Sh. Biloni 2, kusapoti Sekta za Elimu na Afya nchini, kiasi ambacho ni asilimia moja ya faida yao baada ya kodi kwa mwaka 2021, ambayo ni Sh. Bil. 290.
“Changamoto katika Sekta za Elimu na Afya ni kipaumbele chetu, ndio maana NMB iko bega kwa began a Serikali, tunachofanya ni kuangalia tu maeneo gani tunaweza kuisapoti Serikali, ambayo kimsingi inafanya kazi kubwa na leo tuko hapa kukabidhi msaada wenye thamani ya Sh. Mil. 20 kwa shule tatu.
“Tunakabidhi meza na viti 100 kwa Shule ya Sekondari Buguruni Motto, viti na meza 50 kwa Shule ya Sekondari Misitu na madawati 50 kwa Shule ya Msingi Umoja. Tunajua misaada hii haitoshi kumaliza changamoto zilizopo, ila tunawaonesha njia wadau na wafadhili wengine nini cha kufanya katika kuchangia maendeleo,” alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Jumanne Shauri naye aliipongeza NMB kwa namna inavyojitoa kusaidia harakati za kimaendeleo jijini Dar es Salaam, ambako katika kila tukio lenye uhitaji, benki hiyo imekuwa ikijitokeza kuisapoti Serikali, kama ilivyofanya katika Mbio za Mwenge wa Uhuru hivi karibuni.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar, Donatus Richard, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Madawati, Viti na Meza vyenye thamani ya Tsh. milioni 20 kwa Shule tatu za Sekondari za Buguruni Moto, Misitu na Umoja iliyofanyika katika viwanja vya Shule Sekondari Buguruni Moto jijini Dar es SalaamMkuu wa Wilaya ya Ilala Ndatwa Ngwilabuzu (katikati) akipokea sehemu ya Madawati, Viti na Meza vyenye thamani ya Tsh. milioni 20, kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar, Donatus Richard, wakati wa hafla ya makabidhiano hayo kwaajili ya Shule tatu za Sekondari za Buguruni Moto, Misitu na Umoja. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Shule Sekondari Buguruni Moto jijini Dar es Salaam, jana. Kushoto ni Meya wa jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto (wa pili kushoto) ni Diwani wa Kata ya Buguruni, Bosoro Pazi (wa nne kulia) ni MKuruguenzi wa jiji la Dar es Salaam, Jumanne Shauri. Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika hafla hiyo.

Wanafunzi wa Kidato cha kwanza katika Shule hiyo wakitoa burudani ya ngoma ya asili wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndatwa Ngwilabuzu (wa pili kushoto) akipokea sehemu ya Madawati, Viti na Meza vyenye thamani ya Tsh. milioni 20, kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar, Donatus Richard, wakati wa hafla ya makabidhiano hayo kwaajili ya Shule tatu za Sekondari za Buguruni Moto, Misitu na Umoja. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Shule Sekondari Buguruni Moto jijini Dar es Salaam, jana. Kushoto  Diwani wa Kata ya Buguruni, Bosoro Pazi (kulia) ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Buguruni Moto, Mlamu Malawa.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndatwa Ngwilabuzu (katikati) na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar, Donatus Richard, wakikagua sehemu ya Meza, Viti na Madawati wakati wa wakati hafla ya kukabidhi Madawati, Viti na Meza vyenye thamani ya Tsh. milioni 20 kwa Shule tatu za Sekondari za Buguruni Moto, Misitu na Umoja. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Shule Sekondari Buguruni Moto jijini Dar es Salaam, 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.