Habari za Punde

*FOLENI YA DAR YAZUA BALAA MADEREVA WACHAPANA BARABARANI

Dereva wa pikipiki akimkoromea dereva wa gari ndogo aina ya Baruni, aliyembana na kushindwa kupita katika barabara ya Nyerere eneo la Mnazi Mmoja leo. Imeelezwa kuwa foleni hiyo leo imetokana na msafara wa wageni kutoka nchi tofauti waliokuwa wakiwasili nchini kwa ajili ya kuhudhulia mkutano wa Biashara unaotarajia kuanza kesho kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini, ambapo imetolewa taarifa ya kufungwa kwa baadhi ya barabara kwa muda fulani kesho asubuhi ili kutoa nafasi ya kuwapitisha wageni hao watakaokuwa wakihahi katika mkutano huo, hivyo wakazi wa Mbezi na maeneo mengine ambako kuna mahoteli makubwa mnashauliwa kutoka alfajiri siku ya kesho ili msije kukumbwa na foleni la mwaka.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.