Habari za Punde

*WANAFUNZI WA DARASA LA SABA WASOMEA CHINI YA MITI DAR

Wanafunzi wa Darasa la saba wa Shule ya Msingi Mtoni Jijini Dar es Salaam, wakiwa katika masomo yao ya kila siku nje ya madarasani chini miti wakati wakifundishwa na mwalimu wao leo mchana. Walimu wa shule hiyo baada ya kuona kamera ya Sufianimafoto ikiwa kazini walijitetea kuwa wameamua kuwakusanya wanafunzi hao wa mikondo minne na kuwafundisha kwa pamoja, ili waweze kuelewa kwa pamoja kuelekea kujiandaa na mitihani ya darasa la saba ya mwaka huu. Lakini cha kushangaza ni kwamba kama hivyo ndivyo imekuwaje wanafunzi hao wote wafundishwe na mwalimu mmoja je wataweza kuelewa na lengo lao litatimia kweli?
MATATIZO YA OFISI ZA WALIMU BADO NI CHANAGAMOTO...
Walimu wa Shule ya Msingi Twiga ya Jijini Dar es Salaam, wakisahihisha madaftari ya wanafunzi wao wakiwa chini ya miti nje ya madarasa jambo linaloonyesha kuwa shuleni hapo kunaupungufu wa madarsa na ofisi za walimu.

*MADARASA KAMA HAYA KWELI WANAFUNZI WATASOMA KWA BIDII?
Hili pia ni moja kati ya madarasa ya Shule ya Msingi Twiga, kwakweli yanakatisha tamaa kwa wanafunzi kujisomea kwa bidii na hata kwa mzazi anayefika shuleni hapo na kuona mazingira hayo. Hapa mvua ikinyesha ni balaa na naamini ndani ya darasa hili patakuwa hapakaliki, Wadau hebu liangalieni hili kwa macha manne ili tukomboe Elimu ya Tanzania kwani hapa ni ndani ya Jiji kubwa na lenye maendeleo mengi na kila kitu kizuri na zaidi Jiji hili ndilo hasa lenye ofisi za wakuu wote wa nchi hii Je wakuu mnaridhika kweli kuwa na madarasa kama haya katika jiji kama hili? Kama Dar tu ni hivi je Vijijini ni vipi????

Wanafunzi hao wakiendelea kufundishwa na hapa wamepigwa kwa nyuma ili kuonyesha uhalisia wa mahala penyewe na uwingi wao ambao bado wamekatwa kulingana na kamera kwa kweli ni wengi mno.....

Wanafunzi wakiwa katika darasa bovu wakifurahia kupigwa picha....



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.