Habari za Punde

*JK AZINDUA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI DAR

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ,Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia John Mc Intyre (watatu kulia),Waziri wa Miundombinu Dr.Shukuru Kawambwa (kushoto) na Waziri wa TAMISEMI Mhe.Selina Kombani (kulia) wakifunua kitambaa kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Miundombinu ya mfumo wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za uzinduzi zilizofanyika Kivukoni jijini Dar es Salaam leo mchana.

Mtendaji Mkuu wa Mradi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam, Cosmas Takule, akionyesha mchoro wa ramani ya utekelezaji wa mradi huo wakati Rais Jakaya Kikwete, alipozindua mradi huo leo. Kushoto ni Waziri wa TAMISEMI,Selina Kombani, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, John Mc Intyre, (kushoto kwa Rais) ni Waziri wa Miundombinu Dr.Shukuru Kawambwa, wakisikilza kwa makini jinsi ya ujenzi wa miundombinu ya mradi huo. Picha na Freddy Maro




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.