Habari za Punde

*RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA WANANCHI MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 48 YA MUUNGANO

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akipunga mkono kusalimia wananchi wakati akiingia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
 Baadhi ya Viongozi wa Kiserikali wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo katika Uwanja wa Uhuru, wakisimama wakati wa kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Amir Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akikagua gwaride wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar, zilizofanyika leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo katika sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
 Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWT, kikipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo wa haraka na kutoa heshima kwa mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete.
 Kikosi cha Wanamaji kikitoa heshima mbele ya Jukwaa Kuu.
 Kikosi cha FFU kikionyesha uwezo wa kulichapa gwaride kwa mwendo wa haraka.
 Kikosi cha JWT katika mwendo wa haraka.
 Kikosi cha Magereza katika mwendo wa haraka.
  Watoto wa shule mbalimbali za msingi wanaounda kikundi cha alaiki, wakionyesha manjonjo ya michezo na maumbo mbalimbali wakati wa sherehe hizo leo.
  Watoto wa shule mbalimbali za msingi wanaounda kikundi cha alaiki, wakionyesha manjonjo ya mchezo wa Sarakasi.
  Watoto wa shule mbalimbali za msingi wanaounda kikundi cha Halaiki wakionyesha manjonjo ya na kupandisha Bendera ya Taifa.
  Kikundi cha Sanaa cha JKT Oljoro, kikionyesha umahiri wake wa kuimba na kucheza 'Kiduku' wakati wa sherehe hizo.
Baadhi wa wananchi waliofika kushuhudia sherehe hizo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.