Habari za Punde

*UAMUZI WA KAMATI YA RUFANI ZA UCHAGUZI YA TFF

Uamuzi wa Kamati ya Rufani za Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeona haiwezi kuhalalisha uchaguzi ambao tayari ulikuwa umepingwa na mmoja wa wagombea.
“Kuamua hivyo kutazidi kutazidi kulichimbua shimo soka letu,” amesema Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Julius Lugaziya.
Badala yake Kamati ya Rufani ya Uchaguzi, imeagiza kuwa Rufaa ambayo Bwana Tom Mazanda, aliiwasilisha kwenye Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) isikilizwe kwa mujibu wa Katiba na kanuni zake za Chama cha Mpira wa Miguu Kinondoni (KIFA) zinazohusu masuala ya uchaguzi kwa wiki mbili yaani siku 14 kuanzia Agosti 16, 2016 endapo Mrufani bado atataka kuendelea na rufaa hiyo.
Kwa kipindi cha hapa katikati yaani mpito viongozi waliochaguliwa wataingia ofisini na kuendelea na majukumu yao ya kiungozi ikiwamo kusimamia masuala yote ya KIFA mpaka hapo itakapoamualiwa vinginevyo na matokeo ya rufaa iliyoko DRFA.
Uamuzi huo wa Kamati ya Rufaa ya TFF unatokana rufaa iliyowasilishwa kwenye ofisi za TFF na muomba rufani ambaye Juni 12, 2016 alichaguliwa kuendelea kuwa Mwenyekiti wa KIFA, lakini uchaguzi wake huo na wenzake walioshinda ukatenguliwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF mnamo Juni 18, 2016.
Pamoja na kutengua matokeo hayo, kamati iliagiza uchaguzi urudiwe na kuelekeza kuwa hatua mbalimbali za kimaadili zichukuliwe dhidi ya watu walioona waliosababisha sintofahamu katika zoezi la uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.