Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Kamishna wa Polisi (CP) Suzan Kaganda, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika na Asia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Biashara za Kimataifa ya Zimbabwe, Bw. Mqabuko Dube.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika nchini Zimbabwe, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zimbabwe, hususan katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na ushirikiano wa kikanda.

.jpeg)
No comments:
Post a Comment