Menu

Saturday, December 26, 2009

*SIMBA, TUSKER NANI KUJIFARIJI LEO?

Hizi zote ni timu ambazo tayari zimeshaonja joto ya wababe Yanga, na sasa leo zinakutana katika hatua ya kusaka mshindi wa tatu katika michuano ya Kombe la Tusker, je nani atakubari kuwa kibonde kwa pande zote mbili, Tusker walijeruhiwa wiki iliyopita wakati wenzao Simba wamejeruhiwa hivi majuzi tu nadhani wao ndiyo hasa watakuwa na hasira na machungu zaidi na wakihitaji angalau kutopoteza heshima na imani kwa mashabiki wao, mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam leo saa kumi na nusu jioni, wakati Dar Young African itashuka dimbani kesho kuwakabiri Sofa Paka ya Kenya katika Fainali za michuano hiyo.
Lakini Sofa Paka nao bado wanatamani kuendeleza Historia yao na wakitamani isiharibike kwa vyovyote vile kutokana na wao waliweza kupanda daraja msimu uliopita huko kwao nchini Kenya na wakaweza kufanya vyema na hatimaye wakachukuwa ubingwa wa Ligi na kuingia katika michuano hii na bado wameweza kuendelea kufanya vyema.
Je, na wao bado wataweza kuendeleza historia hiyo mbele ya Wababe wa Papic? mwamuzi wa mechi hizo zote mbili yaani ya leo baina na Simba na Tusker na ya kesho ya Yanga na Sofapaka, ni dakika 90 za mchezo mimi na wewe tutasubiri matokeo.

Kikosi cha Sofa Paka

Kikosi cha Simba

No comments:

Post a Comment