Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Veta, Prof. Idrissa Mshoro, (wapili kulia) akielezewa maendeleo ya ujenzi wa Chuo hicho na mjenzi wa Chuo cha Hoteli cha Veta, kinachojengwa Njiro nje kidogo ya mji wa Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Eng. Zebadiah Moshi akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Veta, Prof. Idrissa Mshoro, (Kushoto) kutembelea Chuo cha Hoteli cha Veta, kinachojengwa Njiro nje kidogo ya mji wa Arusha. Mwenyekiti huyo na wadau wa Veta, walifanya ziara ya ukaguzi wa mendeleo ya ujenzi wa chuo hicho mjini Arusha mwishoni mwa wiki.
Jengo la Chuo Cha Hoteli YA Veta linavyoonekana kwa mbele.. Na SPM Repoter
Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi, VETA, imejipanga kuwa mkombozi wa Sekta ya Utalii nchini, kwa kujenga uwezo kwa Watanzania, kumiliki soko la huduma za watalii ambalo kwa sasa, linamilikiwa na wageni zaidi kuliko Watanzania wenyewe.
Hayo yamebainishwa mwishoni mwa wiki, na Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Eng. Zebadiah Moshi, wakati akiwatembeza wadau mbalimbali wa sekta ya utalii, kwenye Chuo cha Utalii cha Veta, kinachotarajiwa kukamilika hivi karibuni, kilichoko mkoani Arusha, ambacho kitatoa mafunzo ya huduma za utalii na uongozi wa hoteli.
Eng. Moshi amesema, soko la huduma za Utalii linakuwa kwa kasi kubwa kunakopelekea ukosefu wa wahudumu wenye utaalamu wa kati na wa juu wa kuhudumia mahoteli ya kitalii, hali inayopelekea ajira nyingi za kati za za juu kushikiliwa na wageni toka nchi jirani, huku Watanzania tukijikuta kama watazamaji.
Eng. Moshi, amesema kwa muda mrefu kumekuweko na upungufu wa wahuduma na watalaamu wa hoteli na huduma za utalii kwenye mahoteli yetu, ni kwa kutambua hitaji hili, ndipo Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi, VETA, ilipoamua kujikita katika ujenzi wa chuo cha kisasa cha mafunzo ya hoteli na huduma za watalii.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Veta, Prof. Idrissa Mshoro, amesema uamuzi wa VETA kujikita kwenye utoaji wa mafunzo ya hoteli na kuhudumia watalii, umefikiwa kwa kuweka maslahi ya Taifa mbele katika jukumu zima za kujenga uwezo kwa Watanzania kutawala biashara ya utalii kinyume cha hali ilivyo sasa kwa wageni kushika nafasi za juu kutokana na kuwepo kwa Watanzania wachache wenye utaalamu huo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Veta kanda ya Kaskazini, Angelus Ngonyani, amesema chuo hicho kimejengwa Arusha karibu zaidi na soko la utalii, na kitatoa mafunzo ya cheti na Diploma za huduma za Utalii na Uendeshaji wa Hoteli na kitajikita zaidi katika utoaji wa mafunzo kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kuendesha hoteli ya kisasa ya kuhudumia watalii .
Wenyeviti na wajumbe toka kwenye kanda zote 9 za VETA, Wenyeviti wa Kamati za Kiufundi za Ushauri (TACs) na wadau mbalimbali wa sekta ya Utalii walitembelea kujionea hatua mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi nchini VETA katika medani za Utalii.

No comments:
Post a Comment