Menu

Thursday, January 14, 2010

*MATUKIO MBALIMBALI YA JIJINI DAR KATIKA PICHA LEO

9Waliokuwa watuhumiwa wa kesi ya kudaiwa kufanya uporaji kwa kutumia siraha katika Benki ya NBC tawi la Ubungo Dar es Salaam, na kupora mamilioni ya fedha wakifurahia mara baada ya kuachiwa huru kwa kesi moja kati ya zilizokuwa zikiwakabili, katika Mahakama ya Hakim mkazi Kisutu Dar es Salaam. Picha na (SPM)

*VIVAZI VYA HATARI KATIKATI YA JIJI LA DAR CITY CENTER...

Wakati mwingine dada zetu muwe mkiangalia vivazi vyenu mahala pa kuvivalia na wakati gani mnatakiwa kuvaa, nahisi huyu dada alijihisi anaingi Bills kwa muda huo kumbe alikuwa akikatiaza katikati ya mitaa ya City Centre Posta, na kumuacha kila aliyepishana naye akigeuza shingo kuhakiki kivazi hicho, hata kama ni joto ama jua kali lakini tukumbuke maadili ya Watanzania jamani, pichani (kushoto) mdada huyu akiwa na wenzake waliovalia nguo za heshima sijui yeye hajishtukii kukatiza mitaani na kivazi hicho tena mchana kweupeeeeee!...

*SERENGETI WAKANUSHA KUHUSIKA NA UJIO WA TIMU YA UGANDA NCHINI.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Serengeti, Teddy Mapunda (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana*, alipokiwa akikanusha kuhusu kutohusika na ujio wa Timu ya Taifa ya Uganda nchini kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki na Ivory Coast. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Tanzania, (TFF), Frederick Mwakalebela, (kualia) Ofisa Habari wa TFF, Florean Kaijage.


*IDRISA AIAGA MTIBWA SUGAR SASA KUKIPIGA SOFAPAKA NCHINI KENYA.


Beki wa Mtibwa Sugar, Idrisa Rajabu (kulia) akiagana na mratibu wa klabu hiyo Jamal Bayser leo mchana alipokuwa akiondoka nchini kuelekea nchini Kenya kujiunga na mabingwa wa nchini humo, Sofapaka. Katikati ni mmiliki wa timu hiyo, Elly Kalekwa aliyekuja nchini kukamilisha mipangpo ya kumnyakuwa beki huyo.

*WASANII WA BONGO WAKAMILISHA SINGLE YA PAMOJA YA KAMPENI YA MARALIA.

Wasanii wa muziki wa Kizazi kipya na Msanii Mkongwe wa miondoko ya Taarab, Bi Kidude (wapili kushoto) wakiimba na kucheza kwa pamoja wimbo wa tangazo la Kampeni ya ‘Malaria Haikubaliki’, wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo uliofanyika jijini leo mchana. Wasanii hao wanatarajia kufanya onyesho la pamoja la kuzindua kampeni hiyo kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni Februari 13 mwaka huu, ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Rais Jakaya Kikwete. Picha na (SPM)


No comments:

Post a Comment