Menu

Friday, January 1, 2010

*WABONGO WALIVYOPAGAWA NA MKESHA WA MWAKA MPYA

Heri ya mwaka mpya, ni furaha kuuona mwaka 2010........Mashabiki wa Bendi ya Akudo Impact, wakisebeneka na miondoko ya bendi hiyo wakati wa shambla shambla za kuukaribisha mwaka mpya, kwenye Ukumbi wa Vatcan City Sinza Dar es Salaam jana usiku.

Hawa ni mashabiki wa Bendi ya Fm Academia nao wakisebeneka na sebene kuukaribisha mwaka mpya, kwenye Ukumbi wa Makumbusho.

Wanenguaji wa Bendi ya Akudo Impact, wakishambulia jukwaa wakati wa onyesho lao la kuukaribisha mwaka.

Wapiga Gita wa Akudo, wakifanya vitu vyao jukwaani.

Wanamuziki wa Fm Academia, wakishambulia jukwaa, yaaaani ilikuwa ni furaha tuuuuuu!!!!!

Meneja wa Bendi ya Akudo Impact, Michael Andrew, (kulia) akimlisha keki kiongozi wa bendi hiyo, Christian Bella, wakati wa onyesho maalum la sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya 2010, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Vatcaan City Sinza.

Meneja wa Bendi ya Akudo Impact, Michael Andrew, (wapili kulia) akikata keki iliyoandaliwa maalum na bendi hiyo kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya 2010 wakati wa onyesho hilo.

Wanamuziki wa Akudo wakishambulia jukwaa, yaaani ilikuwa ni kupekecha tuuuuuuu!!!!!!!.

"Sisi ni Kanisani tu ndo sebene letu na mafunzo ya mheshimiwa Kakobe".....Waumini wa Kanisa la Kakobe lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye Ibada ya kuukaribisha Mwaka Mpya 2010 jana usiku.

Waandishi wa TBC1, wakifanya mahojiano na Kiongozi wa Bendi ya Akudo Impact, Christian Bella, wakati wa onyesho la Mkesha wa mwaka Mpya.









No comments:

Post a Comment