Immaculate, akiwa katika chumba cha Idara ya Habari MAELEZO leo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari alipokuwa akikabidhiwa zawadi ya Kompyuta na Chuo cha Utalii na Maendeleo ya Hoteli (Clever College)
Waandishi wa habari wakimzonga Baba Mzazi wa Immaculate, David Mosha, wakati akitoa historia fupi ya mtoto wake tangu alipoanza elimu ya msingi.
Mwakilishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Doroth Mwaluko (kulia) akimkabidhi Bahasha ya fedha taslim Sh 100,000, Immaculate Mosha, ikiwa ni pongezi kutoka kwa Chuo cha utalii na Maendeleo ya Hoteli, (Crever College) kwa kuwa mshindi wa kwanza Tanzania nzima aliyefanya vizuri katika masomo ya Sayansi kwenye mtihani wa kidato cha nne 2009. Katikati ni Mama yake mzazi, Agatha Mosha, Mkuu wa Chuo hicho, Deborah Nyamlundwa.
"Ebwanaeeeeh kumbe ya ukweli"????? ama kweli kusoma kuzuri.....
Immaculate akiangalia Kompyuta yake aliyokabidhiwa kama zawadi ya kumpongeza, ikiwa na thamani ya Sh. 350,000.
Immaculate (kuli) akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari kwa kujiamini. Katikati ni Baba yake mzazi, David Mosha na Mama yake mzazi, Agatha Mosha.
Immaculate, akiwa na baadhi ya wanafamilia yake, Baba, Mama, Kaka zake na Dada zake, mara baada ya mkutano na waandishi wa habari.
Immaculate, akiwa na Baba na mama yake, pamoja na Mkuu wa Chuo cha Utalii, na baadhi ya wanafunzi wa Chuo hicho, wakipiga picha ya kumbukumbu, mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment