Habari za Punde

*YANGA YATUMIA NYUNDO YA KILO 100 KUUA MENDE












Hivi ndivyo ubao wa magoli ulivykuwa ukionekana mara baada ya mchezo wa Yanga na Toto Africa ya Mwanza kumalizika kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam leo jioni. Kesho Yanga itashuka dimbani katika uwanja huo huo kukipiga na timu ya Zesco ya Zambi ikiwa ni mchezo wa kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa marudiano na Fc Lupopo, ambapo Yanga inatarajia kuondoka nchini Alhamisi wiki hii tayari kwa marudiano ya mchezo huo.










Aliyewahi kuwa Kocha wa Simba, Twarib Hillar , akipiga simu kuomba msaada baada ya kuzuiliwa na walinzi kuingia kwenye geti la Uwanja wa Uhuru leo jioni kushuhudia mtanange kati ya Yanga ya Dar es Salaam na Torto Africa.












Jerry Tegete wa Yanga (kushoto) akiambaa na mpira baada ya kumtoka beki wa Toto AFrica, , William Busweru, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini leo jioni. Yanga imeshinda mabao 6-0.
"Haya weeee umetinga wavuni, duh!.....









Kipa wa Toto Africa, Hussein Katandula, akijaribu kuokoa mpira uliopigwa langoni mwake kwa Tik Tak na Jerry Tegete (hayupo pichani) na kuandika bao la pili wakati wa kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
"We unapitika kirahisi tu Ngoshaaaaaa"!!!!







Beki wa Yanga Fredy Mbuna (kulia) akimtoka, Maulid Haniu wa Toto wakati wa mchezo huo na kupiga krosi iliyozaa bao la pili.









Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Nurdin Bakar (kushoto) akimtoka beki wa Toto Africa ya Mwanza, William Busweru, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa leo jioni, kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

"Ebwana eeeh! saluti babakeeeeee"..........














Boniface Ambani (kushoto) na Freddy Mbuna, wakishangilia baada ya bao lililofungwa na Ambani.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.