Wafuasi wa Chama kipya, Chama cha Jamii , (CCJ) wakiwa na mabango ya chama hicho nje ya ofisi ya Masajili wa Vyama vya Siasa, wakati walipomsindikiza Mwenyekiti wa Chama hicho Richard Kiabo, kukabidhiwa cheti cha Usajili wa muda na Msajili wa Vyama vha Siasa nchini John Tendwa, Dar es Salaam leo.
*KAMPUNI YA PRECISIONAIR YAZINDUA NDEGE MPYA LEO
Naibu Waziri wa Miundombinu, Ezekiah Chibulunje, akifurahi pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya Kampuni ya Ndege ya PrecisionAir, mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Ndege mpya ya abiria ya Kampuni hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo. Kushoto ni Balozi wa Ufaransa, Jacques Labriolle na Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni hiyo, Michael Shirima (kulia).
*BASI LA ABIRIA LA KAMPUNI YA ABOUD LAUNGUA DAR
Wafanyakazi wa Kampuni ya Ultimet Security, wakizima moto uliowaka na kuunguza basi la Kampuni ya mabasi ya Abood lenye namba za usajili T 291 ATH lililokuwa limeegeshwa ndani ya Kituo Kikuu cha mabasi Ubungo, Dar es Salaam leo jioni. haikuweza kufahamika chanzo cha ajali hiyo ya moto.
*ALAUMIWE NANI MANISPAA AU MIUNDOMBINU MIBOVU?
Wakazi wa jijini Dar es Salaam, wakipita mbele ya maduka yaliyopo Posta, huku wakikwepa maji machafu yanayotoka katika chemba ya maji iliyojaa na kuvujisha maji hayo kiasi cha kuwa kero kwa watu wanaofanya shughuli zao na wapiti njia katika eneo hilo.
*MVUA DAR ZAWA KERO KATIKA BAADHI YA MAENEO
Kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam, baadhi ya maeneo bado yamejaa maji na kusababisha usumbufu kama inavyoonekana pichani eneo la nje ya Soko la Samaki la kivukoni likiwa bado limejaa maji.
*AJALI ZA PIKIPIKI ZAZIDI KUTAWALA DAR
Mkazi wa jijini Dar es Salaam ambaye hakuweza kufahamika jina lake, akiwa amekaa chini hoi baada ya kuanguka na pikipiki aliyokuwa akiendesha katika Barabara ya Shekilango wakati akijaribu kulikwepa gari.
No comments:
Post a Comment