Habari za Punde

* HARUSI YA KISHKAJI NI RAHISI, SAFI NA IMETULIA

"Nani kasema Harusi ni lazima iwe ya gharama"?????
Washkaji Bi Harusi na Bw. Harusi, wakiwa High Table mahala walipoandaliwa kukaa wakati wa sherehe yao ya harusi baada ya kufunga ndoa nyumbani kwa Bibi Harusi huyo, hivi karibuni.
Hawa ni wapambe ama wasimamizi wa sherehe hiyo ya harusi wakiwa eneo la tukio wakati wa sherehe hiyo, huku wakiwa na mavazi sare na viatu vya yeboyebo.

Washkaji wakiondoka eneo la tukio kuelekea katika mapumziko 'Honey-moon', wakitumia usafiri simple wa pikipiki Bodaboda.

Kwa kawaida Wabongo tumezoea kuona ama kushuhudia harusi zinazogharimu kiasi kikubwa cha fedha huku wapambe ndugu, jamaa na marafiki wakitumia muda mwingi kukaa vikao ili kuweza kufanikisha sherehe ya harusi hiyo husika na wengine wakisimama kidete kuhakikisha michango inapatikana kwa wakati na kiwango kilichowekwa na Kamati husika ya sherehe ya harusi.
Lakini hii ni tofauti sana na Jamaa hawa wanaosemekena kuwa ni miongoni mwa Watanzania wasiohitaji makuu wala ushahidi wa watu lukuki na manjonjo ya kila aina, kwa kufunga ndoa ya kifahari.
Imedaiwa jmaa hawa ni kutoka huko pembezoni mwa Tanzania kwa wale ndugu zetu wanaopenda Naniliu wanaopenda kutumia majina ya washkaji wa Porini ‘Wanyama’.
Mdau hebu angalia picha hizi kisha linganisha na harusi ama sherehe za harusi ulizokwisha shuhudia na angalau kwa upungufu jaribu kukumbuka gharama na ulinganishe kwa makadilio harusi hii ya ‘Kishkaji’ imetumia kiasi gani cha fedha.
Mshkaji kaoa Simple, Flowers wake Simple wamepiga yeboyebo chini na mavazi white yanayofanana na kisha baada ya hafla hiyo ya ndo washkaji wakajitia kwenye usafiri wa Pikipiki ‘Bodaboda’ na kuelekea katika Honey-moon yao kwa mapumziko, sasa hebu fikiria kuna maana gani ya kutumia gharama kubwa na manjonjo ili kufanikisha ndoa yako? Hali ya kuwa hata ukiwa kama huyu mshkaji tayari umeoa.

NI RAHISI NA NAFUU KUPITILIZA

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.