SUFIANIMAFOTO

Menu

▼

Saturday, May 29, 2010

*50 CENT KULIKONI? AJIKONDESHA AKONDA?


Washngton Dc, Marekani
NYOTA wa wa muziki wa hip hop wa nchini Marekani ambaye pia ni rapa na kiongozi wa kundi la G Unit, 50 Cent ameshitushwa sana anavyojiona kwa kipindi hiki na jinsi anavyoonekana mbele ya macho ya watu baada ya kupoteza makilo kibao (Uzito) na kukonda kupita kiasi.

50 Cent amesema kuwa ameamua kujikondesha namna hiyo kwa ajili ya kujiandaa kucheza Filamu ya America Football Hero Fighting Cancer, iliyo mbioni kukamilika maandalizi yake.

Aidha Rapa huyo mwenye miaka 34 sasa amesema kuwa , amekuwa akitumia misosi ya majimaji tu kwa muda wa wiki tisa sasa ili aweze kufikia malengo ya jinsi anavyohitaji kuonekana katika Filamu hiyo.
Mkali huyo aliyetamba na kibao cha In Da Club pia jina lake halisi ni Curtis Jackson.

50 Cent anavyoonekana alivyokuwa awali.

Hapa ni baada pia ya kujikondesha.












sufianimafoto Muda: Saturday, May 29, 2010

No comments:

Post a Comment

‹
›
Home
View web version
Powered by Blogger.