Habari za Punde

*BONGO HAKUNA MISHIKAKI JAMANI KWA WENZETU NI NOMA

Ebwana eeh! askari wetu wa usalama barabarani, wa hapa Bongo wamekuwa wakiwakamata madeva wa pikipiki na hasa wale askari maarufu kwa jina la Tigo, ambao wamekuwa wakifuatilia zaidi madereva wanaopakiana zaidi ya wawili katika pikipiki na wale wasio vaa kofia za usalama 'Helmet', je wangebahatika kukutana na dereva kama huyu aliyepakia abiria nane (8) katika pikipiki moja na ikiwa katika mwendo si angebaki akishangaa na asijue wala kuamini alichokiona machoni mwake, hii si mchongo ni photo la kweli lililopigwa huko Ufilipino.

Na huyu mama pia nae ni Komando hebu mcheki alivyoning'inia nyuma ya pikipiki. ilimradi tu mzigo wake ufike salama.

Madent wakitoka kuchukuliwa shuleni na usafiri ambao hulipiwa ada kila mwisho wa mwezi kama ambavyo yanafanya baadhi ya magari yanayotoa duma ya kusafirisha wanafunzi hapa Bongo.

Huyu ni mfanyabishara wa mbogamboga akitoka kununu shambani kuelekea katika eneo lake la biashara kuendelea na biashara.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.