
Baadhi ya wanachama wa Klabu ya Simba, wakiwa katika foleni ya kuhakiki kadi zao kwa ajili ya kuingia katika chumba cha kupigia kura kuchagua Viongozi wa Klabu hiyo, wakati wa ucghaguzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi.

Wanachama wakihakiki kadi zao katika Kompyuta ili kuingia ndani ya chumba cha kupigia kura.

Ukaguzi ulikuwa wa makini zaidi kwani baada ya wanachama hawa kutoka katika eneo hili la kukagua kwa kalamu, walifika katika ukaguzi wa kompyuta na kuhakikiwa tena kwa mara ya pili na kupewa kadi za kuingilia ndani.

Haya ndiyio makasha ya kupigia kura yakiwa eneo la tukio kusubiri kuanza kwa zoezi hilo.

Mmoja kati ya wanachama wa Klabu hiyo akiuchapa usingizi, kutokana na uchovu, usingizi na njaa, kwani eneo hilo hapakuwa na dalili yeyote ya kuuzwa msosi hali ya kuwa baadhi ya wanachama walijihimu kuwahi ili kuwahi foleni ya kujisajili na kuingia ndani kabla ya vurugu. pia kama unavyojua inawezekana wengine wamesafiri kutoka mikoani na kufika jijini Dar alfajiri ili kuwahi tukio hilo.

Hawa pia ni wanachama wa Simba, wakijipatia kifungua kinywa njiani karibu na ukumbi huo pembezoni mwa barabara, wakati walipokuwa wakihaha kusaka msosi na kukutana na muuza Sambusa huyu aliyewasitili angalau kupunguza njaa.

Hawa ni baadhi tu ya wanachama waliofanikiwa kuwahi ukumbini hapo na kufanya usajili mapemwa wakiwa ndani ya ukumbi huo.

Haya ni makasa ya kupigia kura yakiwa mbele ya wanachama hao.

Wanamama pia hawakuwa nyuma katika kuwahi kujisajili ili kumpata kiongozi wanayemhitaji wa Klabu yao ya Simba.

Hawa ni baadhi tu ya wagombea wa nafasi mbalimbali za Klabu hiyo, wakiwa ukumbini humo wakisubiri kukamilika kwa utaratibu. Hata hivyo imeelezwa kuwa muda mfupi tu baada ya Sufianimafoto kutoka ukumbini humo, Michael Wambura alifika ukumbini humo haikujulikana sababu za kufika na jiami kuingia mbele ya wanachama hao ambao alikwisha wachanganya na wengi wao wakawa na hasira naye huku ikitishiwa kusitishwa kwa uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment