Menu

Friday, May 14, 2010

*KCB BENKI YAZINDUA TAWI JIPYA DAR

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Muhammed seif Khatib, akikata utepe kuzindua Tawi la 11 la benki ya KCB, likiwa ni tawi la sita kwa jiji la Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo mchana jijini. Kulia ni Mwenyekiti wa benki hiyo, Peter Muthoka (wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo, Edmund Mndolwa.

Seif Khatib, akifungua jiwe la msingi la benki hiyo, kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete

Msanii wa kikundi cha sanaa cha Idodomya, Salum Matunda, akionyesha umahiri wake wa kucheza sarakasi za maajabu, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tawi jipya la benki ya KCB, lililozinduliwa jijini Dar es Salaam
Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Muhammed Seif Khatib, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa benki hiyo baada ya kuwasili kwenye viwanja vya benki tayari kwa ufunguzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Jorum Kiarie, akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Tawi jipya la benki hiyo lililozinduliwa jijini Dar es Salaam leo mchana.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Muhammed seif Khatib, akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi huo
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.

Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Muhammed Seif Khatib, akisalimiana na mmoja kati ya wahudumu wa Mapokezi katika benki hiyo, Amina Mkwizu, baada ya kuzindua na kuingia ndani ya engo hilo kujionea utendaji kazi.

Seif Khatib (katikati) akijaza fomu ili kufungua Account katika benki hiyo baada ya ufunguzi.










No comments:

Post a Comment