Habari za Punde

*MPIGANAJI ATHUMAN HAMIS AREJEA NCHINI KUTOKA SOUTH KWENYE MATIBABU

Mpigapicha wa gazeti la Habari Leo, Athuman Hamisi akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana usiku, akitoka nchini Afrika ya Kusini ambako alikuwa akiendelea na matibabu toka alipoondoka nchini Septemba 28 mwaka 2008, baada ya kupata ajali wakati akiwa safarini na wenzake wakielekea Kilwa mkoani Lindi kikazi, Athuman amerejea nchini baada ya kupata nafuu ambapo kwa sasa atakuwa akitumia kiti hiki anachokiendesha mwenyewe kwa kutumia umeme. Kulia ni Nesi wake aliyesafiri naye kutoka katika Hospitali aliyokuwa amelazwa huko South, Faith Zondi.

Athuman akijaribu kusimama kwa kutumia mashine ya kiti chake ili aweze kuwano na kusalimiana na rafiki zake waliofika kwenye Uwanja wa Ndege jana kwa ajili ya kumpokea.

Mwenyekiti wa Chama cha wapigapicha za habari, Mwanzo Milinga, akimkabidhi Athuman, zawadi ya kadi ya kumbukumbu baada ya kuwasili.

Athuman, akiendesha kiti chake kuelekea katika gari.

"Karibu Sana mwanangu eeh!"
Baba mzazi wa mpigapicha wa gazeti la Habari Leo, Hamisi Athuman (kulia) akimlaki mwanae huyo Athuman Hamisi wakati alipokuwa akirejea nchini kutoka Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu kufuatia ajali ya gari aliyopata Septemba 12, 2008, akiwa na mpigapicha wa gazeti hili Anthony Siame, wakielekea Kilwa mkoani Lindi kikazi.

Athuman na Nesi wake wakiongozana na watu waliofika kuwapokea kuelekea katika usafiri uliokuwa umeandaliwa.

Watu wakiendelea kusalimiana na Athuman.

Leah Samike, mpigapicha pekee wa kike aliye katika chama cha wapigapicha za habari akisalimiana na Athuman.

Mwakilishi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Matina Nkhulu (wapili kushoto) akisalimiana na Athuman baada ya kuwasili uwanjani hapo.

Sufianimafoto, ambaye pia aliwahi kufanya kazi ofisi moja na Athuman Hamisi The Guardian Ltd, akisalimiana na mpiganaji huyo.

Athuman akipakiwa kwenye gari tayari kuondoka katika Uwanja wa ndege.











No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.