Menu

Monday, May 31, 2010

*POPULAR SPORTS &ENTERTAINMENT YAANDAA BONANZA LA KUKARIBISHA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA JUNI 6

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Popular Sports & Entertainment, Othman Kazi, akionyesha zawadi za washindi watakaoshiriki kwenye Bonanza la Mchezo wa Soka lililoandaliwa maalum kwa kukaribisha michuno ya Fainali za Kombe la Dunia 2010, linalojulikana kama '5 Days to South Africa', litakalofanyika kwenye Viwanja vya TCC Chang'ombe Juni 6 mwaka huu, litakaloshirikisha jumla ya timu 12 za jijini Dar es Salaam, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Bonanza hilo jijini leo mchana. Katikati ni Mshauri wa Siasa wa Ubalozi wa Afrika ya Kusini, nchini, Carol Rath, (kulia) ni mwakilishi wa Cocacola, Jasper Migambile na (kushoto) ni msemaji wa Kampuni hiyo. Cliford Ndimbo.
Othman Kazi (kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa mwakilishi wa PSI, ikiwa ni sehemu ya udhamini wao kufanikisha Bonanza hilo.

NDIMBO AFANYA MAZOEZI YA UKIPA UKUMBINI KUMRITHI KASEJA.
Eti Ndimbo nadai kuwa mazoezi si lazima kufanyia uwanjani ilimradi tu kuwa fiti, na ndiyo maana ameamua kuanza mazoezi 'eti' anataka kumrithi Kaseja baada ya kutunguliwa mfululizo huko Kigali katika mashindano ya Kagame yaliyomalizika hivi karibuni.

"Kumbe ukiwa kipa unainjoi namna hii duh!"
Mazoezi yanaendelea ukumbini humo.....

Mapozi....hapa alikuwa akiigiza 'eti' siku atakayokuwa akitambulishwa rasmi kujiunga na kikosi cha Simba kuchukua nafasi ya Kasenaliu.....

Akipiga picha ya kumbukumbu na doli la FIFA lililokuwapo ukumbini hapo na mshkaji wake.

Huyu ni Shaba Kondo, ambaye amedai kuwa ndiye Meneja wa Ndimbo, na anayeshughulika na mapato tuuuuuu, eti wanaomhitaji Ndimbo wamuone yeye....







No comments:

Post a Comment