Habari za Punde

*WANNE WAKAMATWA KUZUIA MKUTANO WA MBUNGE, WIALAYANI LUDEWA


Na Paul Erasto ,Ludewa
WANACHAMA wanne wa chama cha mapinduzi (CCM) wilayani Ludewa mkoani Iringa wamekamatwa na afisa mtendaji wa kijiji cha Ilinindi kata Madilu humo Dennis Luoga kwa kosa la kumzuia mbunge wao wa jimbo la Ludewa Profesa Raphael Mwalyosi kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji chao cha Ilinindi kwa kudai kuwa ameshindwa kutimiza ahadi zakeTukio hilo lilitokea mwishoni wa wiki muda mfupi baada ya wananchi wa kijiji hicho kumfukuza mbunge wao Prof. Mwalyosi (CCM) ili asihutubie mkutano wa hadhara kijijini hapo kama njia ya kushinikiza kutekelezewa ahadi yao kwanza kama alivyo kuwa amepata kuwaahidi .Mmmoja kati ya viongozi wa madhehebu ya dini ambaye alikuwepo katika mkutano huo alimweleza mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kuwa kitendo kilichofanywa na vijana hao si cha kiungwana kutokana na hatua yao ya kumkatia umeme mbunge huyoAlisema kuwa kabla ya mbunge huyo kufika eneo la mkutano kiliandaliwa kikundi cha kwaya kwa ajili ya kumwimbia mbunge huyo na kusifia utekelezaji wa Ilani ya CCM jambo ambalo wananchi wa eneo hilo walishindwa kuunga mkono hali iliyopelekea kufanya vurugu kwa kukata umeme ili kumzuia mbunge huyo kuwahutubia kabisa .“Sisi kama viongozi wa dini tumesikitishwa na hatua ya vijana hao ila bado tunawakumbusha wana siasa kujenga utamaduni wa kusema kweli ili kuepusha migogoro miongoni mwa jamii wanayoiongoza” Mmoja kati ya vijana hao wa CCM waliokamatwa kwa kumzuia mbunge huyo kufanya mkutano Evaristo Mhagama alisema kuwa Prof. Mwalyosi aliahidi kuwapelekea maji kijijini hapo (Ilininda), jambo ambalo hajalitekeleza hadi sasa. Aidha alisema hatua ya wao kumzuia ni kutokana na kushindwa kuwaongeza wahudumu wa afya katika dispensari ya Kijiji hicho, ahadi ambayo bado hajaitekeleza mpaka sasa japo kwaya hiyo ilionyesha kumpamba kwa kufanya kazi vizuri .“Tumechoka kupewa ahadi hewa,” alisema kwa hasira Luciana Nziku(63)mkazi wa Ilininda huku akiwa amefunga kanga kiunoni “toka tumekuchagua ulikuwa wapi mpaka unakuja leo?”Mbunge Mwalyosi alikwenda kijiijini hapo akiwa ameambatana na Mhe. Benard Libato - Diwani wa Madilu - ambaye naye licha ya kuwasihi wananchi hao wamsikilize mbunge wao walimkatalia kata kata.Wana CCM hao wa Ilininda, walioonekana dhahiri kuchoshwa na ahadi zisizo na utekelezaji, na ndipo walipoamua kuzima umeme na kumwamuru aondoe vipaza sauti vyake.Hata hivyo kutona na vurugu hizo kikundi cha Kwaya cha UVIKANJO kilichokuwa kitumbuize nacho kiligoma kuendelea kumwimbia mbunge huyo kwa kuhofia kichapo kutoka kwa wananchi hao wenye hasira kali . “Tutamwimbiaje mtu asiyetekeleza ahadi zake …kwa sasa hatupo tayari kuendelea kuimba tena”alisikika akisema mmoja wa wana UVIKANJOWana CCM hao waliokamatwa na afisa mtendaji huyo Luoga na kuwekwa mahabusu ya kijiji kwa kutuhumiwa kumfanyia fujo mbunge wao ni pamoja na Deo Mgaya, Joseph Mlowe, na Evaristo Mhagama.Hata hivyo afisa mtendaji huyo wa kijiji Luoga alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alisema kuwa kukamatwa kwa wananchi hao ni utekelezaji wa agizo la mbunge wao kutokana na wananchi hao kuonyesha nidhamu mbaya mbele yake .Mbunge wa jimbo hilo Prof. Mwalyosi amekanusha madai hayo na kuwa kama mtendaji aliwakamata aliwakamata kwa nafasi yake na sio kutumwa na yeye kama mbunge.Prof. Mwalyosi ambaye amekuwa akizunguka katika vijiji vya jimbo lake kwa lengo la kuhamasisha maendeleo na kuwaomba wananchi wamchague tena kipindi kijacho amekuwa akipambana na misuko suko mingi ikiwemo ya kuhojiwa juu ya ahadi zake .Alisema kuwa mradi huo wa maji ni mradi wa benki ya dunia ambao unatekelezwa katika vijiji 10 vya kila wilaya na kuwa kijiji hicho ni kimoja wapo na kuwataka wananchi hao kuwa na subira juu ya mradi huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.