
Vodacom Miss Chang'ombe 2010, Geneviva Emmanuel (katikati) akiwa na washindi wenzake mshindi wa pili, Upendo Urasa (kulia) na mshindi wa tatu, Anna Daud baada ya kutangazwa washindi katika shindano kuwani Taji la Miss Chang'ombe lililofanyika kwenye Viwanja vya TCC Sigara Jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo.

Warembo wakipita jukwaani na vazi la Ufukweni wakati wa shindano hilo.

Mrembo akipita jukwaani na vazi la Ubunifu.

Mrembo akipita jukwaani na vazi la Ubunifu.

Mwandaaji wa shindano hilo Tom Chilala 'Nyabo' (kushoto) akiwa na mgeni rasmi katika shindano hilo Mbunge wa jimbo la Temeke Mh. Abbas Mtemvu, wakifuatilia kwa makini yanayojili jukwaani.

Mashabiki wa fani ya urembo, wakishangilia wakati mmoja kati ya warembo hao aliyevitia kwa kila kitu akipita jukwaani.

Wasanii wa kikundi cha Sanaa cha Mionzi chenye maskani yake Temeke, kikitumbuiza wakati wa shindano hilo.
"Tumekuja kuwapa shavu wenzetu, nasie tulitokea huku"

Kutoka (kushoto) Elsi Martin, Jokate Mwegelo na Sia Ndaskoi, wakiwa katika shindano hilo wakifuatilia kwa makini, hapa wakipozi kwa picha baada ya kuona likamera likiwalenga....

Makamu Mwenyekiti wa Kwanza wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Athuman Nyamlani (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Gazeti la Jambo Leo, Juma Pinto, wakifuatilia kwa makini jukwaani kuona ni nani atakayekuwa Miss Chang'ombe, na hatimaye Miss Temeke na baadaye Miss Tanzania.
No comments:
Post a Comment