Habari za Punde

*WALIMU 10, WANAFUNZI 13, SHULE YA MSINGI NDUGUMBI WAPEWA 'SHAVU' KUIONA BRAZIL





Na Benjamin Sawe-MAELEZO Dar es Salaam

Wanafunzi 10 pamoja na walimu 13 wa Shule ya msingi Ndugumbi iliyopo magomeni, Wilaya
ya Kinondoni wamepewa nafasi ya kushuhudia mchezo wa kirafiki baina ya Taifa Stars na Brazil, siku ya jumatatu wiki ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria nchini.
Nafasi hizo zilizotolewa na Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF), Leodgar Tenga zina lengo la kuhamasisha watanzania kupitia mchezo wa mpira wa miguu ikiwa ni ishara ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria.
Bwana Tenga alisema TFF na mashirika ya African United Against Malaria na Kentaro Group
wamekubaliana kushirikiana katika kupambana na ugonjwa wa Malaria kwa kutumia njia ya
michezo mashuleni kwani mchezo huo umekuwa kipenzi cha watu wengi duniani.
“Bila kutokomeza ugonjwa wa Malaria inamaana hata wachezaji wa Taifa Stars wataugua ugonjwa huu hivyo kusababisha kutofanya vizuri katika michuano mingi kwa sababu ya kuugua na malaria mara kwa mara”.Alisema Bwana Tenga.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Kentoro bwana Phillipe Huber amesema kampuni yake itatoa fulana 100 na mipira kwa katiaka shule ya Ngugumbi iliyopo magomeni ikiwa na lengo la kuhamasisha wanafunzi kupitia michezo ili kupambana na malaria.
Akizungumza kwa niaba ya Shirika la Africa United Against Malaria Mkurugenzi wa Shirika hilo
Bi Christina Barrineau alisema wameanzia kutoa elimu mashuleni kwani wanafunzi watakuwa na
nafasi nzuri ya kuelimisha jamii pindi wanapokuwa watu wazima.
“Unajua kampeni hii ni kampeni ya muda mrefu na tumeanzia kutoa elimu hii mashuleni
kwasababu watoto ukimjenga mtoto vizuri kuhusu jambo fulani atakuwa mwalimu mzuri wa
kuelimisha jamii juu ya athari za ugonjwa wa malaria”.Alisema Bi Barrineau
Akitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya
Ndugumbi Warda Kibuga alisema wanashukuru TFF pamoja na mashirika ya Africa United Against Malaria na Kentaro Group kwa kuwapatia vifaa mbalimbali vya michezo.
“Tunashukuru kwa vifaa mlivyotupatia na tunawahakikishia tutavitumia vifaa hivi vya mpira wa miguu hasa kipindi cha mapumziko wakati wa mazoezi na mechi kwa kutoa elimu ya jinsi ya
kupambana na ugonjwa wa malaria kwa wapinzani wetu na hata sisi wenyewe”.Alisema.
Pia alisema hiyo watakayopata kipindi cha mpira kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali wa
malaria wataisambaza katika jamii ili ipate elimu juu ya kujikinga na ugonjwa huo.

Rais wa TFF, Leodger Tenga na Ujumbe wa Maralia kutoka Brazil, wakipiga pich ya pamoja na waalimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ndugumbi, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo shuleni hapo ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Maralia nchini.

'SI JELA NI DARASANI'
Wanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Ndugumbi Magomeni jijini Dar es Salaam, wakibanana katika dirisha lenye nondo wakigombea kuchungulia nje kumuona Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Leodger Tenga, wakati alipofika shuleni hapo na Balozi wa Maralia kutoka nchini Brazil, Philippe Huber, kwa ajili ya kutoa vifaa vya michezo kwa shule hiyo ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Maralia.
Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Leodger Tenga, akizungumza na wanafunzi, wakati wa hafla hiyo.

Wapiga picha wa vyombo vya habari wakiwa bize kutafuta picha za tukio hilo wakati walipokuwa katika hafla hiyo.

Tenga, akihiojiwa na waandishi wa habari baada ya tukio hilo, (kulia) ni Mwanamitindo, Mustafa Hassanali.





No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.