Askari wa Kikosi cha zima moto 'FIRE', wakijadiliana jinsi ya kuwakamata madereva wote wasiokuwa na vifaa vya kuzimia moto kwenye magari yao, ambapo leo wameweza kuweka kambi ya zoezi hilo katika barabara ya Chang'ombe eneo Chuo cha VETA, jijini Dar es Salaam ili kufanikisha zoezi hilo, ambalo lilianza siku za nyuma katika mtaa wa Ilala Malapa.
*VIVAZI VINGINE HIVI JAMANI HATA KAMA NI WAZUNGU HII NO....
*WAVUVI HARAMA KESI YAO BADO IPO IPO MAHAKA KUU DAR
*EBWANA EE USAFIRI MWINGINE WA HATARI JAMANI
Abiria akiwa na mzigo wa Kompyuta kwenye pikipiki, ambapo mzigo huo ulionekana kumuelemea huku akikosa mahala pa kujishikiza wakati pikipiki hiyo ikiwa kwenye mwendo eneo la Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo mchana, bila kujali usalama wake kwanza na sijui iwapo vifaa hivyo vitaanguka anaweza kutumia gharama gani kuvitengeneza si zaidi ya gharama ambayo angechukulia usafiri wa usalama na kufika kwa usalama mahala anapokwenda????.
Eti jamaa akijificha kuogopa kamera baada ya kuona akitunguliwa mfululizo, kumbe zamaaaani tayari.
*KAHAWA KWA KASHATA KIJIWENI POOOOUWA
Hiki si kijiwe cha Kahawa kwa Msisiri, bali ni mahala tu walipopateuwa baadhi ya waandishi kupumzika nyakati za mchana baada ya kumaliza kazi ili kusubiri usafiri ama kazi nyingine zinazoweza kujitokeza, lakini si kupumzika pekee bali hata kujiburudisha na Gahwa kidogo, Icecream ili kuvuta mua, kama unavyowaona madada hawa Amina (kulia) akijisevia kahawa kwa Kashata si kwamba ndo msosi no, hii ni testa tu jamani.....
*KAHAWA KWA KASHATA KIJIWENI POOOOUWA
No comments:
Post a Comment