Na Hillary, Shoo,Singida.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Mohammed Dewji(MO) leo amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka katika kampeni kugongwa kwa nyuma na gari la mgombea mwenzake, Hawa Ngulume, lililogonga kwa nyuma ya basi hilo dogo.
Ajali hiyo imetokea leo jioni majira ya saa 10 jioni katika eneo la ofisi za Manispaa ya Singida
muda mfupi baada ya wagombea hao kutoka katika kata ya majengo kunadi sera zao kwa wanachama, kwa ajili ya kuwania kuteuliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo lililokuwa likiongozwa na MO baada ya kumaliza muda wake.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa katika hali isiyokuwa ya kawaida
walipatwa na mshangao mkubwa baada ya kuona dreva wa gari aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili T 425 AMK ambaye jina lake bado halijahafahamika kugonga HIACE hiyo yenye namba za usajili T 655 BEB iliyokuwa ikitumiwa na Dewji pamoja na mwenzake aitwae Mariam Mhuwila.
Habari zaidi zinasema kuwa juzi wagombea wote Dewji, Mariam na Ngulume walipanda gari moja lakini jana Ngulume alikataa kupanda gari hilo maalumu kwa ajili ya wagombea na kuamua
kutumia gari lake binafsi.
Katika ajali hiyo Dewji alipata mshituko sehemu ya shingo baada ya gari hilo kugomga kwa
nyuma Hiace hiyo ambapo MO alikuwa amekaa nyuma na kusababisha kupata majeraha na mshituko sehemu ya shingo na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa vipimo vya X ray ilibainika kuwa MO amepata
mshituko sehemu ya shingo na kupatiwa dawa za kuchua kabla ya kuruhusiwa kurejea nyumbania na hali yake inaendelea vizuri.
Kufuatia ajali hiyo dereva wa Mgombe hawa Ngulume anahojiwa na polisi kwa tuhuma ya
kuendesha gari kizembe na kusababisha ajali.
Kamanda wa polisi Mkoani hapa Celina Kaluba amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kwamba
uchunguzi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo na taarifa kamili zitatolewa leo ili hatua
zaidi ziweze kuchukuliwa kwa wahusika.
Juhudi za kumpata Katibu wa CCM Manispaa ya Singida Mary Maziku ili kuzungumzia tukio hilo
hazikufanikiwa hadi tunakwenda kupublish tukio hili.

wananchi wa wakishangaa baada ya ajali hiyo kutokea katika eneo hilo.
Dereva Mgombea ubunge jimbo la Singida mjini Hawa Ngulume mwenye traki suti
nyeusi ambaye hata hivyo jina lake bado halijafahamika akihojiwa na polisi kwenye eneo la
tukio hilo Manispaa ya Singida.
No comments:
Post a Comment