Haya ndiyo hasa magari yenyewe na haya ni sehemu tu kati ya magari 100 yatakayoshindaniwa kwenye Promosheni hiyo.
Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom, Ephraem Mafuru akizungumza na waandishi wa habari kabla ya uzinduzi huo akielezea jinsi ya kushiriki Promosheni hiyo.
mapaparazi wakiwa bize kupiga picha wakati viongozi na wakurugenzi wa Vidacom wakielekea katika magari hayo...
Miss Tanzania Miriam Gerald (katikati) na Dylan Lennox, wakifunua mapazia kufungua sehemu yalipokuwa magari hayo.
Ishara ya uzinduzi huo wote wakiwa na mabango yanayoonyesha tangazo la Promosheni hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu za mkononi Vodacom, Francois Swart (kulia) na Miss Tanzania 2009-2010, Miriam Gerald, wakizindua Promosheni mpya ya ‘Shinda Mkoko’ itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia gari aina ya Hyundai i 10, yenye thamani ya Sh. milioni 10, ambapo yameandaliwa jumla ya magari 100 kwa ajili ya mshindi mmoja kila siku. Kushoto ni Mkurugenzi Masoko wa Vodacom, Ephraem Mafuru, (kulia) ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na wateja, Aika Matiku.
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu za mkononi Vodacom, Francois Swart (kulia) akikata utepe kuzindua Promosheni mpya ya ‘Shinda Mkoko’ itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia gari aina ya Hyundai i10 yenye thamani ya Sh. milioni 10, ambapo yameandaliwa jumla ya magari 100 kwa ajili ya mshindi mmoja kila siku. Wakwanza (kushoto) ni Mkurugenzi Masoko wa Vodacom, Ephraem Mafuru (katikati) ni Miss Tanzania 2009-2010, Miriam Gerald.
Baadhi ya wakazi wa Jijini Dar es Salaam waliohudhulia hafla hiyo ya uzinduzi huo katika Viwanja vya Mlimani City leo mchana.
Baadhi ya wakazi wa Jijini Dar es Salaam waliohudhulia hafla hiyo ya uzinduzi huo katika Viwanja vya Mlimani City leo mchana.
No comments:
Post a Comment