Wachezaji wa Yanga, wakipasha kabla ya kuanza kwa mcezo huo, nyuma yao ni Ubao ukionyesha idadi ya magoli kuwa bado ni 0-0, lakini hadi mwisho wa mchezo huo ubao huu ulibadilika.
Baadhi ya waandishi wa habari, waliotoka jijini Dar es Salaam, hadi visiwani humo kwa ajili ya kuripoti mechi hiyo, wakiwa jukwaani kabla ya kuanza kwa mcezo huo, huku wakiwa wamejichanganya na mashabiki, jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa na waandishi hao kila kukicha kuchanganywa na mashabiki ni hatari.
Rais wa Zanzibar, Dk. Mohammed Ali Shein, akimkabidhi Nahodha wa timu ya Simba,Nico Nyagawa, Kikombe cha ushindi baada ya mchezo huo kumalizika katika uwanja wa Amani mjini Zanzibar jana usiku ambapo Simba iliibuka kidedea kwa kuifunga Yanga mabao 2-0, katika fainali za Kombe la Mapinduzi.
Nyagawa akifurahia na Kikombe baada ya kukabidhiwa kombe hilo pamoja na Kitita cha fedha Sh. milioni 5.
Wachezaji na Mashabiki wa SImba, wakishangilia na kikombe hicho uwanjani hapo.
Beki wa Simba Meshack Abel, akifurahia na Kikombe hicho.
Beki wa Simba Meshack Abel, akifurahia na Kikombe hicho.
Mussa Hassan Mgosi, akishangilia goli lake alilofunga kipindi cha kwanza.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao lililofungwa na Mussa Hassan Mgosi kipindi cha kwanza.
Idd Mbaga wa Yanga (kushoto) na Meshack Abel
Mashabiki wakizozana kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Ubao wa Matangazo ukionyesha goli la kwanza la Simba, katika kipindi cha kwanza ambapo kipindi cha pili ubao huu ulibadilika na kusomeka 2-0.
Mashabiki wakizozana kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Ubao wa Matangazo ukionyesha goli la kwanza la Simba, katika kipindi cha kwanza ambapo kipindi cha pili ubao huu ulibadilika na kusomeka 2-0.
No comments:
Post a Comment