Msanii wa kizazi kipya Jaffaray,maaruf kama Jaffarhymes, ametangaza rasmi katika ukurasa wake wa 'FACE BOOK' kuwa si muda mrefu kuanzia sasa ataachana na aliyekuwa mpenzi wake na mchumba wake aliyeishi naye kwa kipindi cha miaka nane, ambaye alitarajia kufunga naye ndoa.
Jaffarayy ambaye hakuweza kuweka wazi sababu za kuchukua hatua hiyo ameandika kwa kifupi sana taarifa hiyo na kuwafanya watu kibao kukoment katika ukurasa huo na kuchangia kila mmoja akitoa lake kuhusu uhusiano wa wapenzi hao.
No comments:
Post a Comment