Bondia Awadhi Tamim, mtanzania anayeishi nchini Sweden, akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dara es Salaam leo mchana, kwa ajili ya pambano lake la kutetea mkanda wake wa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati uzito wa 'Havy weight', kati yake na Ashraf Suleiman, linalotarajia kufanyika machi 5 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee. Tamim, ametamba kumchakaza Ashraf na kuonyesha mcheo wa kimataifa zaidi ambapo amesema amejipanga kumuonyesha mpinzani wake Panchi za uhakika na kuwahakikishia mashabiki wake kuwa mkanda huo ataondoka nao tena bila ubishi wala maswali kwani pambano hilo hatarajii kulifikisha mbali ili ushindi wake usiwe wa utata kama ambavyo iliwahi kutokea wakati alipopambana na mpinzani wake huyo siku za nyuma na hatimaye pambano likavunjika kutokana na fujo.
CAF YAONGEZA ZAWADI LIGI YA MABINGWA AFRIKA WANAWAKE
-
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeongeza zawadi za ushiriki wa michuano
ya Ligi ya Mabingwa kwa Wanawake barani kwa asilimia 52 na sasa litatumia
kiasi...
3 hours ago
No comments:
Post a Comment