Mara kadhaa madereva wa magari makubwa yanayosafiri usiku na mizigo ama mafuta, wamekuwa wakikumbwa na tatizo la kuibiwa mizigo njiani usiku kutokana na wezi wanaokuwa pembezoni mwa barabara katika baadhi ya maeneo nyakati wa usiku na hasa maeneo ya milima na kona ambapo hupanda juu ya gari wakati likiwa katika mwendo na kushusha mizigo. Kutokana na madereva hao kusumbuliwa na wezi wa aina hiyo hivi sasa wamebuni mbinu kama hii ya kuweka miba nyuma ya gari ili kuwafanya wezi kuogopa miba hiyo pindi wanapotaka kupanda gari hilo na kuiba, kama linavyoonekana gari hili pichani.
Msajili wa Hazina azindua Mpango Mkakati wa NMB 2026–2030
-
Na Mwandishi wa OMH
Dar es Salaam. Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, amezindua Mpango
Mkakati wa Muda wa Kati wa Benki ya NMB wa mwaka 2026 hadi 2...
2 hours ago
No comments:
Post a Comment