Habari za Punde

*MATEMBEZI YA MAJI 'TIGO WALK FOR WATER' KUFANYIKA APRIL 16 MLIMANI CITY DAR


Meneja Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya ‘Spearhead Africa Ltd’, Bertha Ikua, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu matembezi ya Maji ‘Tigo Walk For Water 2011’ zinazotarajia kufanyika Aprili 16 mwaka huu katika Viwanja vya Mlimani City kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia miradi ya maji na juhudi za wazalendo kutatua janga la maji linalowakabili wakazi wa Bagamoyo, Katikati ni Ofia Uhusiano wa Kampuni ya simu za Mkononi Tigo ambao ni wadhamini wakuu, Jackson Mmbando na Msemaji wa Tigo wa Walk For Water, Jakate Mwegelo.


*****************

WALK FOR WATER 2011- MWAKA WA PILI WA JUHUDI ZA WAZALENDO KUTATUA JANGA LA MAJI LINALOWAKABILI TAKRIBAN WAKAZI 100,000 WA BAGAMOYO.

Baada ya mafanikio makubwa ya Dow Live Earth Run for Water 2010- sehemu ya mradi wa kimataifa wa kutatua tatizo la janga la ukosefu wa maji ulimwenguni kote, kampuni ya simu za mkononi tiGo Tanzania pamoja na Spearhead Africa Limited inaamini kwamba mwamko huu upewe kipaumbele kwa kuzingatia kwamba janga hili la ukosefu wa maji bado halijatokomezwa. Huu ni mwaka wa pili kwa shughuli hii ya uchangajishaji fedha kuendeshwa nchini na kampuni ya Spearhead.


Lengo la shughuli hii kwa mwaka huu ni kuchimba visima vyenye urefu wa mita 200 na 100 ili kutoa ufumbuzi kwa zaidi ya wakazi 100,000 waishio Bagamoyo ambao hawana uwezo wa kupata maji safi na salama.


Mwaka huu kampuni ya simu za mkononi ya tiGo imejitolea kusimamia shughuli nzima ya Walk for Water na kampuni ya Spearhead na imefurahia mchango huo wenye lengo la kutokomeza janga hili. tiGo Tanzania kama moja ya wadhamini wa Dow Live Earth Run for Water 2010, pamoja na kuona mwamko wa wananchi kujitokeza kwa wingi kutokomeza janga hili, tiGo wameamua kutoa msaada huu kama sehemu ya huduma zao kwa jamii ambayo imewazunguka.


Malengo ya matembezi haya ya hisani ni:


1. Kutaarifu umma na wadau wa maji kuhusu janga la maji na ufumbuzi wa janga hili.


2. Kutoa fursa kwa wadau wote wa maji kutoa elimu ya kutunza maji ,matumizi mazuri ya maji na kutoa taarifa kuwa ni wajibu wa kila mmoja wetu kusaidia kutatua janga hili.


3. Kuhamasisha mashirika kushiriki kwenye mbio/matembezi ya hisani, kuonesha bidhaa au huduma zao na kutoa mchango kwa mradi teule wa naji.


4. Kuchangisha fedha kwa ajili ya mradi endelevu wa maji utakaotoa huduma kwa jamii kwa muda mrefu.


Afisa uhusiano wa Tigo Tanzania, Mr. Jackson Mmbando alisema,” Tunafuraha kuwaletea shughuli hii ya kuchangia mradi wa maji na tunawahamasisha waandaaji wengine kuwa na moyo kama huu. Pia hii sio changamoto tu kwa Bagamoyo bali kwa maeneo yote ya Tanzania. Tunawahimiza wachangiaji na watu binafsi kujisajili na kuchangia mradi huu.


“Kupitia Tigo Walk for Water, tunatarajia kupata fedha taslim shiligi Milioni 60 za Tanzania kwa ajili ya mradi huu, kwa msaada wa Ifakara Health Institute, tumeweza kutambua maeneo ya kuyapa kipaumbele ya kuchimbwa visima vyenye urefu wa mita 200 na 100 ili kuipatia jamii maji salama katika kata za Bagamoyo.”


tiGo Walk for Water itafanyika kwenye uwanja wa maegesho ya magari ya Mlimani City Mall siku ya jumamosi, 16 Aprili 2011. “Tunawashukuru Tigo kwa kutuletea shughuli hii ya kuchanga fedha. Tunategemea wale wote walioshiriki mwaka jana kwenye uwanja wa taifa watatuunga mkono kwa kujisajili kwa matembezi au mbio za kilometa 6, umbali ambao unakadiriwa ni wastani wa umbali wanaotembea wanawake wengi na watoto kila siku kutafuta maji safi ya kunywa.” alisema Bertha Ikua- Meneja Huduma kwa wateja wa Kampuni ya Spearhead Africa.


Mradi wa maji wa Bagamoyo iliyopo chini ya Ifakara Health Institute ndio utakaonufaika na Tigo Walk for Water 2011.


Bertha Ikua aliongezea “Kuna vijiji vingi Bagamoyo ambavyo wananchi wake hawawezi kupata maji safi na salama.Visima vingi ni vifupi na vinakauka wakati wa kiangazi, mito siyo salama na ipo mbali na makazi ya watu, maji ya mvua ni ya msimu na maji ya bomba ni kwa ajili ya watu wachache wenye uwezo wa kulipa bili ya kila mwezi.


Baadhi ya maeneo ambapo kina cha maji ni kirefu, mara nyingi ni rahisi kuchimba visima venye sifa ya ubora kwa gharama nafuu lakini maeneo ambayo kina cha maji ni kifupi tutahitaji kuchimba vissima venye vina virefu zaidi ya mita 100 ili kupata maji.”


Usajili wa mtu binafsi kwa ajili ya matembezi ya maji ni shilingi 3000 na usajili huo utaanza tarehe 28 Machi katika Makao Makuu ya Tigo yaliyopo barabara ya Nyerere na mtaa wa Ohio, Shoppers Plaza Masaki na Mikocheni, City Supermarket iliyopo Harbour view, Shoprite ya barabara ya Pugu, Village Supermarket iliyopo Sea Cliff Village, Novel Idea yiliyopo mtaa wa Ohio, maduka na ofisi zote za hoteli ya Oysterbay pamoja na Mlimani City Mall.


Kampuni mbalimbali, Balozi, mashirika ya serikali na yasiyo ya kiserikali yanahamasishwa kushiriki siku hii kwa kuifanya iwe siku ya pamoja ya wafanyakazi na kujisajili kutembea kwa pamoja kama kampuni au shirika kupitia anuani ya barua pepe kahenga@spearheadafrica.com au kwa kupiga simu 0713 252 254.


Asilimia 50 ya ada ya kujisajili na maonesho na asilimia 100 ya michango yote itapelekwa kwenye mradi wa maji.


Wadhamini wakuu wa tiGo Walk for Water ni Tigo Tanzania, na wadhamini wengine ni Konyagi na AngloGold Ashanti- Geita Gold Mine pamoja na support sponsors wengine, ambao ni: Uhai, Hugo Domingo, Image Masters, Digital, A1 Outdoor, Mlimani City, Ultimate Security, Synovate, Davis & Shirtliff, Africa Beat, Advertising Dar, M2 Advertising na BMTL.


Shughuli hii ya tiGo Walk for Water 2011 imechukua sura tofauti ikilinganishwa na mwaka jana. Mwaka huu kutachezeshwa droo ya bahati na sibu siku hiyo baada ya kukimbia au kutembea. Zawadi zitatolewa kwa washindi baada ya kuchezeshwa droo hiyo kutokana na fomu zao za usajili. Hivyo ukijisajili unapata nafasi ya kuweza kushinda zawadi ambazo zimetolewa na Tigo, Samsung, Ideal Computers, Mr. Price, Little Impression, Movenpick na wengineo.


“Nina ipa moyo familia yangu, marafiki, wanamuziki, wanaminitindo na watu wengine mbalimbali mashunguli pamoja na wenzangu wote kuniunga mkono katika mpango huu. Sote kwa pamoja tutembee na kukimbia ili tusaidie kuweka utofauti kwa namna moja au nyingine katika kubadili hali hii, siyo tu kwa ajili yetu pekee bali pia kwa watoto wetu. Jitokeze leo kujisajili,kuchangia na kufanya maonesho.” Alisema Miss Jokate Mwagelo ambaye ni balozi wa matembezi ya maji ya tiGo 2011.


-MWISHO-


Kuhusu tiGo


tiGo ni kampuni ya kwanza ya simu za mkononi Tanzania, ilianza shughuli zake mwaka 1994,ni mtandao wa gharama nafuu na ubunifu wa hali ya juu kiutendaji.



tiGo ni sehemu ya Millicom International Cellular S.A (MIC) ,inatoa huduma kwa gharama nafuu na hupatikana kirahisi katika maeneo mengi, pia inaurahisi wa kulipiwa huduma ya kabla kwa wateja wa zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanayoibuka Afrika na Latin America.


Mafanikio ya tiGo yamejikita katika msingi wa mkakati wa “Triple A” ambao unasimama badala ya Affordability, Accessibility na Availability. Tunatengeneza ulimwengu ambao huduma za simu za mkononi unakuwa nafuu na unapatikanaji wake ni rahisi mahali pote na kwa watu wote. Hii inatoa dhamana kwa wateja wetu ambao wanapata huduma bora kwa gharama nafuu katika mikoa yetu yote 26 ya Tanzania Bara na Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.