Habari za Punde

*KIKOMBE CHA BABU WA LOLIONDO CHAIBUKIA IRINGA

Na Francis Godwin, Njombe Iringa

WAGONJWA mbalimbali wamemiminika nyumbani kwa Dkt Antony Mwandulami (58) mkazi wa kijiji cha Itunduma Wangama wilaya ya Njombe mkoa wa Iringa kupata dozi ya bure ya vikombe vitatu vya dawa kama ya babu wa Loliondo .

Baadhi ya wagonjwa waliopata dozi hiyo kwa babu wa Loliondo na kufanikiwa kupata na dozi hiyo kwa Mwandulami wametoa ushuhuda na kusema kuwa kikombe hicho si kama cha Mbeya ila ni kama cha Loliondo . Baadhi ya watu wameweza kutoa ushuhuda wao kama Nery Kasoli (50) mkazi Mbeya mjini ambaye alikuwa na na Hilda Asenga (30) aliyekuwa asumbuliwa na kichaa na kutoongea kwa muda kipindi kirefu ambaye sasa amepona . Alisema kuwa binti yake huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo kwa muda wa miaka takribani 10 ila baada ya kupata kikombe mtoto wake huyo amepona na anazungumza vizuri kabisa. Huku Issa Omary (45) yeye alidai kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na kutibiwa katika hospitali mbali mbali za seikai bila mafanikio na baada ya kunywa kikombe hicho hali yake ni nzuri na jana amekwenda kupima Hospitali ya Ikonda ameonekana ni salama.

Wengine waliotoa ushuhuda wao jana ni pamoja na kijana mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Kevin ambaye anadai kuwa alikuwa akisumbuliwa na HIV ila sasa amepima na kuonekana ni salama. Akizungumza na waandishi wa habari waliofika nyumbani kwake kushuhudia zoezi hilo la utoaji wa dozi ya vikombe vitatu ,Mwandulami alisema kuwa lengo la kuanza kutoa bure dawa hiyo ni kutaka wagonjwa kutoa ushuhuda zaidi wao baada ya kunywa dawa hiyo badala ya vyombo vya habari na watoa huduma hiyo kuendelea kujitangaza zaidi na kujisifia kwa jambo ambalo si geni.

Mwandulami ambaye ni mshauri mkuu wa waganga wa tiba asilia Tanzania ameanza kutoa kikombe hicho ijumaa ya wiki iliyopita na kudai kuwa mti huo hajaotoshwa na Mungu wala mizimu bali alionyeshwa na marehemu baba yake zaidi ya miaka 18 iliyopita na sasa amekuwa akiutumia mti huo aina ya Makhirikhiri kwa kuchanganya na miti mingine.

Hata hivyo Mwandulami yeye amekuwa akitoa dozi hiyo kwa kutumia kikombe cha udongo huku kikombe na cha Plastiki amekuwa akitumia kugawia dawa hiyo ambayo huiweka katika ndoo kubwa ya lita 60 na kutoa dozi hiyo bila malipo yeyote.

“Naomba sana wagonjwa wangu wanaofika kupata kikombe ambao wanatumia dozi za UKIMWI kwa sasa kuendelea kutumia dozi hizo ….hadi serikali itakapo tuma timu ya madaktari kuja kuchunguza dawa hii na kujua idadi ya magonjwa inayotibu kama na UKIMWI upo” , alisema Mwandulami.

“Babu wa Loliondo ni kama amenifunua kwa kiasi japo mimi na yeye bado mimi ni mkongwe zaidi yake na ushuhuda wa wagonjwa wanaofika kupata tiba hapa na wale waliopatiwa tiba ni ukweli zaidi ya wale wa Loliondo ambao hata miezi mitatu haijamalizika, mimi hapa nimeanza kutoa huduma hii miaka zaidi ya 17 sasa.

Nadhani kitu nilichokuwa nikikosea mimi ni kuchanganya na miti mingine ndio maana wagonjwa walikuwa wakipona kwa kasi ndogo ila toka ijumaa nilipoanza kuchemsha mti huu peke yake mafanikio makubwa nimeyaona kwa wagonjwa sugu kupata nafuu” Alisema.

Alisema dawa yake imekuwa ikitibu kwa siku tatu baada ya kumaliza dozi ya vikombe vitatu ambapo kila mwezi ni kikombe kimoja na kuwa kwa sasa bado hajapanga ni kiasi gain kwa mgonjwa aweze kulipia ila mbele ya safari kila kikombe kitakuwa shilingi 2000.
*********************** Baadhi ya wakazi wa Njombe Mkoani Iringa, wakiwa katika harakati za kupata kikombe kwa Mwandulami.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.