SHABIKI wa damu wa timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Rashid Mchata, amegojiwekea mgomo wa kutosikiliza redio, kununua magazeti na kwenda Baa kwa muda wa siku tano mfululizo kuanzia jana, baada ya timu yake ya Simba kushindwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Mchata amefikia hatua hiyo baada kuwa na matumaini lukuki kuwa huenda timu yake ingeweza kuibuka na ushindi wa mabao lukuki ilipocheza na Majimaji ili iweze kufikisha ushindi wa mahesabu na kuwapiku watani wao wa jadi Yanga, jambo ambalo halikuwezekana kwani hadi mchezo huo unamalizika Simba 4 na ikaruhusu kufungwa goli 1.
Wakati shabiki huyo akiwa na matumaini hayo yaliyeyushwa na makelele ya mashabiki wa Yanga waliokuwa wakishangilia kila bao lililofungwa kwenye uwanja wa Kirumba wakisikiliza uwanjani hapo kupitia matangazo ya redio na hadi mwisho wa mchezo huo Yanga ikaweza kuibuka na ushindi wa mabao 3 na haikuweza kuruhusu kufungwa hata goli moja.
Akizungumza na Sufianimafoto kwa njia ya simu, Mchata alisema kuwa toka jana anaogopa hata kununua gazeti la Mtanzania, Nipashe na Mwananchi kwani anaojua akigeuza nyuma ya magazeti hayo atakutana na habari za michezo ambazo kwa siku hizi tano kuanzia jana kwake ni kama anajichoma mkuki wa tumbo.
“Nasema hiviiiiiiii, sinunui ng’ooooo, magazeti ya michezo na hata ya kawaida kwani nayo yanahabari za michezo kwa nyuma, na wala sisikilizi redio wala kuangalia Tv kwa muda wa siku tano hadi machungu yapungue” alisema Mchata Mchata hufikia hatua hata anapokwenda Baa na kukuta viti vya Njano hugoma kukaa na kumwita mhudumu ili kumtafutia kiti cha rangi nyekundu ama rangi nyingine tofauti na njano ama kijani. Ebwana eeeh! Shabiki huyu ni Noma hadi amepitiliza jamani duh!
No comments:
Post a Comment