Pichani ni sehemu ya ramani, ya kitalu namba 4 iliyo na usajili na 38383, E' 353/107 toleo la tarehe 24/05/2004 inayoonyesha kuwa kiwanja no, 30 ni eneo la wazi. Eneo la Mivumoni Mkoani Mbeya, limevamiwa na watu wanaojiita wawekezi katika maeneo ya wazi, ambao wamekuwa wakiwalaghai wananchi wakijiita ni wawekezaji wanaotarajia kufanya biashara na siku chache maeneo hayo ambayo hata hivyo si rasmi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi, ambayo ni maeneo ya wazi huonekana nyumba zikiendelea kujengwa na wawekezaji hao kwa ajili ya makazi, jambo ambalo limewashtua wananchi.
Kiwanja na 30 chilichopo kitalu namba 4,kikiwa kimezungushiwa uzio na mwekezaji aliyejulikana kwa jina moja la Msaki. Wakazi ya maeneo hayo walifanya usafi wa eneo ili kuwawezesha watoto kucheza katika kiwanja hicho lakini huyu aliyejiita mwekezaji alifika na kuanza ujenzi wa nyumba na kuzungushia uzio. Kwa mujibu wa meelezo yake yeye ni mmiliki halali wa eneo hilo .
No comments:
Post a Comment