Habari za Punde

*KITUO CHA REDIO YA SWEET FM YA MBEYA CHATEKETEA KWA MOTO

KITUO cha redio cha Sweet Fm, kilichopo jijini Mbeya kimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia jana na kusababisha hasara kubwa.

Joachim Nyambo, kutoka Mbeya, anaripoti kuwa, Mkurugenzi wa kituo hicho Joseph Mbuza, amezungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia jana na kusema kuwa kuungua kwa studio ya redio hiyo kumesababisha hasara ya mamilioni ya fedha.

Hata hivyo chanzo cha moto huo bado hakijajulikana japo inahisiwa kuwa ni hitilafu ya umeme huku thamani halisi ya mali zilizoteketea katika studio hizo bado kupatikana.

Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wahabari Mkoani Mbeya Christopher Nyenyembe, alisema kumekuwa na matukio mengi ya nyumba na ofisi mbalimbali kuteketea kwa moto unaosababishwa na hitilafu za umeme usiokuwa wa uhakika ambao unakatikakati mara kwa mara na hivyo kuwasababishia hasara kubwa wananchi.

Nyenyembe, alisema matukio hayo yanapotokea wananchi ndio wamekuwa wakipata hasara huku Tanesco ambayo inawajibika na suala la usambazaji umeme likishindwa kuwalipa fidia wahusika kutokana na kutokuwepo kwa mikataba na wateja wao.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.