Habari za Punde

*SHINDANO LA MISS IRINGA KUFANYIKA LEO

KITENDAWILI cha kumsaka Vodacom Miss Iringa 2011, kinatarajia kuteguliwa leo katika ukumbi wa Highlands mjini Iringa ambapo jumla ya warembo 8 kati ya 14 walioteuliwa katika mchujo, wanatarajia kupanda jukwaani jioni ya leo kutoana jasho katika kuwania taji hilo.
Mratibu wa shindano hilo, Edwin Bashir, alisema kuwa maandalizi yote ya shindano hilo tayari yamekamilika na kuongeza kuwa warembo wengine zaidi ya 6 wameenguliwa katika shindano hilo kutokana na utovu wa nidhamu.
Aliwataja washiriki wa taji hilo kuwa ni ,Ritha Justine (20)Christina Wiliam (21), Christina Bange(20), JaQuelene Erick (21), Happniness James (21), Ursula Hepelwa(20), Belinda Lugenge (20),Zay Mselemu (20) .

Aidha alitaja zawadi za washindi wa kinyang'anyiro hicho kuwa ni, mshindi wa kwanza ni shilingi 700,000 ,mshindi wa pili shilingi 500,000,mshindi wa tatu shilingi 300,000 huku mshindi wa nne na watano watapata shilingi 100,000 kila mmoja na wengine kifutajasho cha shilingi 50,000.

Shindano hilo litasindikizwa na wasanii mbali mbali akiwemo Khadija Kopa ,Rama D na Steve R&NB ambapo wadau wa urembo watashuhudia onyesho hilo kwa kiingilio cha kati ya shilingi 10,000 na 15,000 na onyesho hilo kurushwa Live katika blogu ya Francis Godwin.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.