Habari za Punde

*KUNYWA POMBE KUPITA KIASI NI HATARI KWA AFYA YAKO,' ULEVI NOMAAAAAAAAA'

 Watoa huduma wakibeba mwili wa mtu mmoja kati ya watatu aliyefariki waliokutwa humba Namba 425 kwenye Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam leo.
Imeelezwa kuwa mtu huyo aliyekutwa amekufa ni raia kutoka Zambia, ambaye inadaiwa kuwa kifo chake ni kunywa pombe kupita kiasi, huku wenzake wawili wakikutwa hoi na kupelekwa Hospitali ya Muhimbili kwa matibabu.
Aidha imeelezwa kuwa watu hao wote mbao ni wanaume wamekutwa katika Chumba hicho kilichopo Ghrofa ya nne, ambacho kilikuwa kimekodishwa na raia wa Uingereza.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alisema kuwa mpaka sasa hawajaweza kubaini undani wa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.
Mmoja kati ya watu hao aliyepata fahamu akiwa katika Hospitali yaMuhimbili ni Raia wa Uingereza, aliyejitambulisha kwa jina la Eliud Sikwabi, aliyewataja wenzake kuwa ni Ikbar Bahabur, ambaye ni raia wa Zambia pamoja na Mtanzania aliyetajwa kwa jina moja la Omar.

Imeelezwa kuwa watu hao walikuwa ni miongoni mwa wageni waliokuwa wamehudhuria katika Harusi ya Mtoto wa Mark Bomani, Clement, ambapo walianza kupombeka katika sherehe hiyo na hatimaye wakaendeleza funda jingine baada ya kufika hotelini hapo.
Mwili wa aliyefariki ukipakizwa katika gari. Picha na Stori hii ni kwa Hisani ya Blog ya Michuzi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.